Pata taarifa kuu

Uingereza yaahidi kuipa Ukraine silaha zaidi

Nairobi – Uingereza imeiahidi Ukraine silaha zaidi kwa ajili ya mapambano yake dhidi ya Urusi, wakati huu Rais Volodymyr Zelenskyy akikutana  na waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.

Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Ukraine  Volodymyr Zelensky nchini London mwaka jana
Waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky nchini London mwaka jana © AFP - JUSTIN TALLIS
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya Sunak ilisema kwamba Uingereza ilikuwa tayari kuthibitisha kuwa inaipa Ukraine makombora zaidi ya ulinzi wa anga, pamoja na ndege zisizo na rubani za masafa marefu zenye umbali wa zaidi ya kilomita 200 (maili 124).

Hatua hiyo inaonyesha kuwa Uingereza iko katika mstari wa mbele zaidi kuliko nchi nyingine yoyote katika kutoa silaha zenye uwezo wa kuinua uwanja wa vita kwa upande wa Ukraine.

Zelenskyy, katika safari yake ya pili nchini Uingereza tangu Urusi ilipovamia nchi yake Februari 2022, alimshukuru mshirika wake mkuu na kusema kwamba vita hivyo ni suala la usalama sio tu kwa Ukraine na ni muhimu kwa Ulaya yote.

Ukraine inaendelea kujiandaa kwa mashambulizi ambayo yanatarajiwa dhidi ya majeshi ya Urusi na anayosema yatakua hatari zaidi katika juhudi za kuiokomba miji yake.

Siku chache  zilizopita Zelenskyy alitembelea Ufaransa ,Ujerumani na Italia  katika juhudu za kutafta msaada zaidi ili kuiokomboa nchi yake .

Mzozo kati ya Urusi na Ukraine ulianza Febrauri 2014, ukihusisha vikosi vya wanaotaka kujitenga vinavyosaidiwa na Urusi kwa upande mmoja, na Ukraine kwa upande wa pili. Mzozo huo unahusu hasa hadhi ya Crimea na Donbas.

Kwa mara ya kwanza tangu aingie madarakani, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alifanya ziara ya kiserikali mjini Kyiv Jumamosi tarehe 19 Novemba mwaka jana. Alichukua fursa hiyo kukutana na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, na kumthibitishia uungaji mkono wa Uingereza kwa Ukraine na ambao unaonekana sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.