Pata taarifa kuu

Rais wa Ufransa ,Emmanuel Macron akutana na Tajiri Elon Musk jini Paris

Nairobi – Rais  wa ufaransa Emmanuel Macron amekutana na  tajiri mkubwa duniani ,bilionea Elon Musk hii leo jijini Paris  kujadili miradi ya baadaye ya uwekezaji, wakati kiongozi huyo wa Ufaransa akiandaa mkutano unaolenga kuwashawishi viongozi katika sekta ya biashara kuwekeza pesa zao nchini Ufaransa.

Elon Musk akutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jijini Paris
Elon Musk akutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron jijini Paris AFP - MICHEL EULER
Matangazo ya kibiashara

Macron alimkaribisha tajiri wa pili duniani, ambaye ni mhusika mkuu wa kampuni ya magari ya kielektroniki ya Tesla, kampuni ya mitandao ya kijamii ya Twitter na kampuni ya uchunguzi ya anga ya SpaceX, miezi sita baada ya kukutana kwa mara ya mwisho nchini Marekani.

Macron na Musk walikutana katika Ikulu ya Elysee kabla ya wote wawili kuelekea Versailles kwa toleo la hivi punde zaidi la mkutano wa rais wa Chagua Ufaransa ambapo Macron anataka kuchagiza uwekezaji nchini humo.

Waziri wa Fedha Bruno Le Maire aliambia shirika la utangazaji la BFMTV kwamba "mazungumzo yanaendelea" na mkuu huyo.Hata hivyo Le Maire hakutoa maelezo ya mazungumzo ya hii leo na Musk, akisema tu kwamba "uwekezaji wote wa leo ni matunda ya miezi au hata miaka inayokuja".

Miezi kadhaa iliyopita Elon Musk alihakikisha, katika mahojiano na BBC kwamba usimamizi wa Twitter umekuwa sawa na "milima ya Urusi" na kutambua "makosa mengi", miezi sita baada ya kuinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 44. 

Uuzaji huo ulibadilisha kampuni kubwa ya mitandao ya kijamii iliyokuwa inafanya biashara ya umma na kuwa kampuni ya kibinafsi, inayomilikiwa na Musk pekee, tajiri mkubwa duniani.

Musk ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya kutengeneza vyombo vya kurushwa angani SpaceX, awali alisema Twitter inatakiwa kuwa kampuni ya kibinafsi ili iimarishe uwezo wake kwa ajili ya uhuru wa kujieleza.

Baada ya kununua hisa za kampuni hiyo ya Twitter, Musk alijitambulisha mwenyewe kama “mtetezi mkubwa wa uhuru wa kujieleza.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.