Pata taarifa kuu

Rais Zelensky yuko ziarani mjini Rome Italia

NAIROBI – Rais wa Ukarine Volodymyr Zelensky yuko mjini Rome ambapo anatarajiwa kufanya mkutano na waziri mkuu Giorgia Meloni na kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, Hii ikiwa ni ziara ya kwanza kwa kiongozi huyo nchini Italia tangu  nchi yake ilipovamiwa na Urusi.

Rais wa Ukraine anazuru Rome Italia
Rais wa Ukraine anazuru Rome Italia AP - Gregorio Borgia
Matangazo ya kibiashara

Rais Zelensky amethibitisha kuwasili kwake mjini Rome kupitia ukurasa wake wa twitter ambapo alilakiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Italia Antonio Tajani.

Aidha kiongozi huyo pia amethibitisha kwamba atafanya kikao na rais wa Italia Sergio Mattarella, waziri mkuu Giorgia Meloni na Papa Francis.

Televisheni nchini humo zimeonyesha msafara mrefu wa magari yaliombeba rais Zelensky yakiondoka katika uwanja wa ndege, maofisa wa usalama wakonekana pia kufunga sehemu kubwa ya mji mkuu wa Italia.

Wakati rais Zelensky akiwasili mjini Rome, Ujerumani imetangaza msaada wa silaha zenye kima cha euro bilioni 2.7 kwa ajili ya Kyiv, msaada huo ikijumuisha magari ya kivita na silaha ya za kuzuia mashambulio ya angani.

Wakati Zelensky akiwasili mjini Rome, Ujerumani imetangaza msaada wa silaha wa kima cha euro bilioni €2.7 kwa Ukraine
Wakati Zelensky akiwasili mjini Rome, Ujerumani imetangaza msaada wa silaha wa kima cha euro bilioni €2.7 kwa Ukraine © FRANCE 24

Licha ya nchi ya Italia, mwanachama wa EU na NATO kuonekana kuwa na uhusiano mzuri na Moscow, nchi hiyo imetuma silaha kwa Ukraine tangu uvamizi wa Urusi mwezi Februari mwaka wa 2022.

Kando na kutuma silaha nchini Ukraine, Italia pia imeonekana kuunga mkono vikwazo vya kiuchumi vilivyotangazwa na mataifa ya Magahribi dhidi ya Urusi.

Meloni, waziri mkuu wa Italia, alifanya ziara nchini Ukraine mwezi Februari ambapo alikutana mwenzake wa Kyiv  Denys Shmyhal.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Tarehe 9 Februari  2023
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na waziri mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Tarehe 9 Februari 2023 AP - Johanna Geron

Taarifa za karibu kwa ziara hiyo zinasema kuwa huenda rais Zelensky akazuru Ujuerumani baada ya kumaliza ziara yake mjini Rome.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.