Pata taarifa kuu

Iran yawaachia huru Raia wawili wa Ufaransa waliokua wanashikiliwa kwa mashtaka ya Usalama

Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Catherine Colonna amesema kuwa Iran imewaachia huru raia wawili wa Ufaransa , Bernard Phelan na Benjamin Brière waliofungwa katika kesi tofauti na  kwa sasa wapo safarini kurejea Ufaransa.

Bernard Phelan na Benjamin Brière waachiwa huru na mahakama ya Iran
Bernard Phelan na Benjamin Brière waachiwa huru na mahakama ya Iran AFP - HANDOUT,-
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao walikuwa miongoni mwa raia wa kigeni waliofungwa jela nchini Iran  na ambao wafuasi wa kisiasa wanaona kama mateka wanaoshikiliwa katika mkakati wa kimakusudi wa Tehran kupata makubaliano na nchi za Magharibi.

Phelan, 64, na mshauri wa usafiri wa Paris, alikamatwa mwezi Oktoba huko Mashhad na amekuwa akishikiliwa tangu wakati huo.

Mnamo Aprili, alifungwa jela miaka sita na nusu kwa mashtaka ya usalama wa kitaifa yaliyopingwa  vikali na familia yake.

Familia ya Phelan ilisema afya yake ilizorota sana akiwa kizuizini. Phelan aligoma kula mnamo Januari kupinga kuzuiliwa kwake lakini akasimamisha hatua hiyo kwa ombi la familia yake, ambayo ilihofia angekufa.

Briere, 37, alizuiliwa kwa mara ya kwanza akiwa safarini nchini Iran Mei 2020 na baadaye akahukumiwa kifungo cha miaka minane jela kwa kosa la ujasusi.

Kisha aliachiliwa na mahakama ya rufaa lakini alibaki gerezani katika hali iliyochukuliwa kuwa "isiyoeleweka" na familia yake.

Akiwa ameshikiliwa kama Phelan katika gereza la Vakilabad huko Mashhad, Brière pia aligoma kula ili kupinga masharti yake.

Raia wengine wanne wa Ufaransa, waliotajwa hapo awali kama "mateka" na wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa, bado wanazuiliwa gerezani na Iran.

Colonna alisema alizungumza mapema Ijumaa na mwenzake wa Iran Hossein Amir Abdollahian na kuweka wazi "azimio la Ufaransa la kuhakikisha kwamba raia wengine wa Ufaransa ambao bado wanazuiliwa nchini Iran pia wanapata uhuru wao haraka."

Wizara ya mambo ya nje ya Iran pia imesema wawili hao wamezungumza kwa njia ya simu kuhusu kuachiliwa kwa Briere na Phelan, jambo ambalo ilieleza kuwa ni "hatua ya kibinadamu".

Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema kuachiliwa kwa mateka hao ni vyema  huku akiapa "kuendelea kufanya kazi kwa ajili ya kurejea kwa wenzetu ambao bado wanazuiliwa nchini Iran".

Dublin vile vile imesema "ilipumzishwa" na kuachiliwa kwa Phelan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.