Pata taarifa kuu

Rais Putin ameongoza sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet

NAIROBI – Rais wa Urusi Vladimir Putin anaongoza sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi. Sherehe hizi zinafanyika wakati huu Urusi ikiwa inaendelea kupigana vita nchini Ukraine

Rais wa Urusi Vladimir Putin anaongoza sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi.
Rais wa Urusi Vladimir Putin anaongoza sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi. AP - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya ushindi wa vita vya pili vya dunia dhidi ya wapiganaji wa kinazi, kiongozi huyo amesema kuwa lengo kuu la mataifa hayo ni kuhakikisha kuwa nchi yake inaporomoko.

Aidha rais Putin ameeleza kuwa nchi yake inataka kuwepo kwa amani katika siku zijazo japokuwa nchi za Magahribi zimeendelea kupanda kile anachodai ni mbegu za chuki dhidi ya raia wa taifa lake.

Wanajeshi wa Urusi wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi
Wanajeshi wa Urusi wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi REUTERS - TATIANA MEEL

Vile vile rais Vladmir Putin, anasema hatma na nchi yake iko mikononi mwa wanajeshi wanaopigana nchini Ukraine, akieleza kuwa anajivunia wanajeshi wake amabao wanaendelea kushiriki na kupambana na katika kile ambacho amekuwa akitaja kama operesheni maalum ya kijeshi ya Urusi nchini Ukraine.

Katika hotuba yake mkuu huyo wa nchi ya Urusi ametoa wito kwa kila raia wa nchi yake kuwaunga mkono wanajeshi hao ambao amewataja kama mashuja wa nchi ya Urusi.

Raia wa Urusi wakiwatazama wanajeshi wa nchi hiyo wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi
Raia wa Urusi wakiwatazama wanajeshi wa nchi hiyo wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi REUTERS - TATIANA MEEL

Rais Putin kwa muda sasa amekuwa akirejelea kauli yake ya kuilinganisha serikali ya Ukraine iliyochaguliwa kupitia njia ya kidemokrasia na Wanazi walioshindwa katika vita vya pili vya dunia.

Putin aidha amewashutumu viongozi wa Ukraine kuwa Wanazi mamboleo. Moscow imekuwa ikizituhumu nchi za Magahribi ambao ni washirika wa Ukraine kwa kuchangia katika mzozo unaoendelea kati yake na Kyiv.

Wanajeshi wa Urusi wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi
Wanajeshi wa Urusi wakati wa sherehe za kusherekea ushindi wa muungano wa Kisoviet dhidi ya wapiganaji wa Kinazi AP - Alexander Zemlianichenko

Naye Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kuwa umoja wa ulaya haufai kutishwa na matamshi ya Putin na maonyesho ya uwezo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.