Pata taarifa kuu

Waziri wa mambo ya nje wa China atoa wito wa 'kuimarisha uhusiano' na Marekani

Nairobi – Waziri wa Mambo ya Nje wa China Qin Gang amefanya mazungumzo na balozi wa Marekani hii leo na kusema kuwa , kipaumbele kikuu ni kuleta utulivu kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu.

Waziri wa mambo ya nje wa China atoa wito wa 'kuimarisha uhusiano' na Marekani
Waziri wa mambo ya nje wa China atoa wito wa 'kuimarisha uhusiano' na Marekani REUTERS - ALY SONG
Matangazo ya kibiashara

Majadiliano ya Qin na Nicholas Burns huko Beijing ni moja ya mikutano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili tangu Washington ilipopiga puto inayodaiwa kuwa ya kijasusi ya China juu ya Marekani mapema Februari.

Tukio hilo lilipelekea Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kusitisha ghafla safari adimu ya kwenda China.

Qin alimwaambia Burns kwamba uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulikuwa wa "umuhimu mkubwa", lakini kwamba "msururu wa maneno na vitendo potovu vya upande wa Marekani" umedhoofisha maendeleo yao tangu Rais Xi Jinping wa China alipokutana na mwenzake wa Marekani Joe Biden huko Bali Novemba mwaka jana.

Qin alielekea Ulaya siku ya Jumatatu, ambapo atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock na mwenzake wa Ufaransa Catherine Colonna, kabla ya kuelekea Norway.

  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.