Pata taarifa kuu

Ukraine yatuhumiwa kuwa na njama ya kutaka kumuua rais Vladmir Putin

NAIROBI – Urusi imeishtumu Ukraine kwa kujaribu kutumia ndege yake isiyokuwa na rubani kwa lengo la kumuua, rais Vladimir Putin.

Muonekano wa Kremlin ya Moscow huko Moscow, Urusi, Jumatano, Mei 3, 2023.
Muonekano wa Kremlin ya Moscow huko Moscow, Urusi, Jumatano, Mei 3, 2023. AP
Matangazo ya kibiashara

Haya ni madai makubwa zaidi tangu Moscow ilipoivamia Kiev mwaka mmoja uliopita.

Madai haya yametolewa na serikali jijini Moscow na kuripotiwa na vyombo mbalimbali vya Habari vya ndani na nje ya nchi hiyo.

Hata hivyo, shutuma hizi zimekanushwa na Mykhailo Podolyak  mshauri wa Ukraine ambaye amesema nchi yake haihusiki na haifahamu lolote kuhusu madai ya serikali ya Urusi.

Taarifa zaidi kutola Moscow, zinasema ndege hiyo isiyokuwa na rubani ilikuwa imelenga makaazi ya rais maarufu kama Kremlin, lakini rais Putin hakuwepo wakati wa jaribio hilo.

Moscow inasema, kitendo hicho ni cha kigaidi na jaribio la kumuua kiongozi wake wa nchi na ina haki ya kulipiza kisasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.