Pata taarifa kuu

Watu 13 wauwawa nchini Ukraine baada ya shambulio baya la Urusi.

Nairobi – Urusi imefanya mashambulio baya katika miji yote  nchini Ukraine na kusababisha vifo vya watu 13 wakati huu Kyiv ikijiandaa kwa makabiliano makali ili kurejesha eneo lao linalokaliwa na nchi hiyo.

Watu 13 wauwawa nchini Ukraine
Watu 13 wauwawa nchini Ukraine © REUTERS - PAVLO PALAMARCHUK
Matangazo ya kibiashara

Lengo kuu la Kyiv  kujiandaa kwa makabiliano ni kujaribu kurejesha tena eneo linalokaliwa na Urusi.Hivi karibuni, Urusi ilipunguza kufanya mashambulio makubwa nchini Ukraine, tofauti na kipindi cha baridi ambapo ilikuwa ikishambulia miundombinu ya taifa hilo jirani.

Nchi hiyo imefanya mashambulio ya anga nchini Ukraine kwa kipindi cha karibu miezi miwili.

Waziri wa mambo ya ndani, Igor Klymenko, amesema mashambulio katika mji wa kusini mwa Kyiv yamewaua watu 10 wakiwemo watoto wawili.

Rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky amelaani vikali mashambulio haya na kuapa kujibu kile alichokiita ugaidi wa Urusi, wakati mapigano makali yakishuhudiwa zaidi katika eneo la mashariki mwa taifa hilo, ambako wanajeshi wanakabiliana ili kuudhibiti mji wa Bahkmutambao kwa sasa unaonekana kama mahame baada ya kuharibiwa vibaya.

Mapigano yameshuhudiwa tangu Urusi ilipoivamia Ukraine mwaka 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.