Pata taarifa kuu

NATO kuendelea kuisaidia Ukraine: Jens Stoltenberg

NAIROBI – Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ameendelea kutoa wito kwa Jumuiya ya Jeshi la nchi za Magharibi NATO kuikaribisha na kuipa msaada zaidi wa silaha kuendelea kupambana na Urusi.

Jens Stoltenberg katibu mkuu wa NATO na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Jens Stoltenberg katibu mkuu wa NATO na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky AP - Efrem Lukatsky
Matangazo ya kibiashara

Zelensky ametoa kauli hiyo mbele ya Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg aliyezuru Kiev ambaye amesisitiza kuendelea kuisaidia Ukraine.

Hii imekuwa ziara ya kwanza ya Stoltenberg nchini Ukraine, baada ya Urusi kuivamia nchi hiyo mwaka mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa Ukraine, hatua ya Urusi kuvamia ardhi yake ni ishara tosha ya kuunga mkono azma yao ya kuijiunga na muungano huo wa NATO, Zelensky akionekana kughabishwa na kile anachosema washirika wake nchi za magharibi hajaweka wazi ni linin chi yake itapewa unachama wa NATO.

Jens Stoltenberg ni katibu mkuu wa NATO

"Lengo kuu na muungano wa NATO ni kuhakikisha kuwa Ukraine inashinda na inaendelea kuwa taifa huru na la kidemokrasia barani Ulaya." alisema Jens Stoltenberg.

Moscow kwa upande wake imekuwa ikiona hatua ya Ukraine kujiunga na NATO kama tishio ikionya dhidi ya juhudi hizo.

Aidha Urusi imeeleza kuwa hatua ya nchi za NATO kuihami Ukraine na silaha za kijeshi ni ishara kuwa muungano huo na Marekani zinapigana na Moscow kupitia Ukraine.

Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg
Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg NATO

Alhamis ya wiki hii, Kremlin ilisema kuwa kuzuia Ukraine kuijiunga na NATO inasalia kuwa mojawapo ya lengo lake na kuivamia Kyiv.

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa akidai kuwa hakuwa na lengine la kufanya ila kuwatuma wanajeshi wake nchini Ukraine kuzuia nchi hiyo kujiunga na NATO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.