Pata taarifa kuu

Urusi: Mkosoaji wa Putin afungwa jela miaka 25

NAIROBI – Urusi imemfunga jela miaka 25, Kara-Murza ambaye ni mkosoaji wa rais Vladimir Putini kwa makosa yanayohusishwa na uhaini. Hatua hii inakuja wakati huu Kremlin ikionekana kuwalenga wapinzani tangu Moscow ilipoivamia Kyiv

Kara-Murza,Mkosoaji wa rais Putin
Kara-Murza,Mkosoaji wa rais Putin REUTERS - Joshua Roberts
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wanahabari waliohudhuria kikao cha mahakama jijini Moscow, Kara-Murza mwenye umri wa miaka 41, alipatikana na kosa uhaini pamoja na kusambaza taarifa za uongo kuhusu jeshi la Urusi.

Kwa sasa Kara Murza mwenye uraia wa Urusi na Uingereza anakuwa mwanasiasa wa kwanza hivi karibuni miongoni wengine wengi ambao ni wapinzani na wakosoaji wa utawala  wa rais Putin kukamatwa na kuzuiliwa na maofisa wa polisi wengine wakilazimika kutoroka nchini humo kwa hofu ya kuzuiliwa.  

Mpinzani huyo wa Putin amekuwa akionekana kutokubaliana na sera na mabadiliko yanyotekelewa na utawala wa Kremlini akikosoa vikali kesi na mashtaka dhidi yake.

Wakati akiwa mahakamani wiki jana Kara Murza aliiambia mahakama mjini Moscow kwamba “anaamini kila neno nililolisema."

Pamoja na kukosoa kile kinachoitwa "operesheni maalumu ya kijeshi" nchini Ukraine, Kara-Murza pia alizungumza wazi wazi dhidi ya rais Vladimir Putin na hatua yake ya  kuwakamata wapinzani.

Murza alikuwa na nafasi kubwa katika kuzishawishi serikali za Magharibi kuwawekea maafisa wa Urusi vikwazokwa ukiukaji wa haki za binadamu na ufisadi. Uingereza kwa upande wake imeitaka Moscow kumuachia huru Kara-Murza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.