Pata taarifa kuu

Ufaransa: Mahakama ya Katiba yaidhinisha kwa ujumla mageuzi ya pensheni

Wazee wa Busara wa Montpensier, ambao maoni yao yalisubiriwa kwa hamu, wamekataa vifungu sita vilivyotolewa katika mageuzi ya pensheni yaliyofanywa na serikali ya Ufaransa, ikiwa ni pamoja na 'kiwango ch juu'. Lakini kwa vifungu vingine, kwa muhtasari mpana, na hasa kuhusu kusogezwa mbele kwa umri wa kisheria hadi 64, sehemu kubwa ya mradi imeidhinishwa. Wazo la kura ya maoni kupigwa pia limekataliwa.

Mwanajeshi wa Ufaransa akitoa ulinzi mbele ya Mahakama ya Katiba nchini Ufaransa, Ijumaa hii, Aprili 14, 2023.
Mwanajeshi wa Ufaransa akitoa ulinzi mbele ya Mahakama ya Katiba nchini Ufaransa, Ijumaa hii, Aprili 14, 2023. AFP - IAN LANGSDON
Matangazo ya kibiashara

"Usiku wa leo, hakuna mshindi wala mshindwa", amesema Elisabeth Borne, baada ya Mahakama ya Katiba nchini Ufaransa kuidhinisha mageuzi yake ya pensheni, sawa, kulingana na Waziri Mkuu, na 'mwisho' wa 'mchakato wa kidemokrasia' wa nakala hii iliyolenga 'kuhifadhi mfumo wetu wa malipo kama unavyokwenda".

Mahakama ya Katiba imeidhiniisha mageuzi mengi yaliyofanywa na Waziri Olivier Dussopt hasa, na kwa hivyo kusogezwa mbele kwa umri wa kisheria wa kustaafu kutoka miaka 62 hadi 64. Hatua hii, iliyolalamikiwa kwa miezi kadhaa na waandamanaji walioingia mtaani kila mara, kwa hivyo itakuwa na nguvu ya sheria mara tu Emmanuel Macron atakapotia saini na kuwa sheria, wakati vifungu sita vya pili vimefutwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.