Pata taarifa kuu

Mlipuko wa jengo Marseille: Mwili wa mtu wa nne watolewa chini ya vifusi

Siku moja baada ya mlipuko wa jengo na kuporomoka kwa jengine katikati mwa Marseille, miili ya watu wanne imepatikana chini vifusi. Kazi ya uokoaji bado ni hatari na ni ngumu. "Bado kuna matumaini" ya kupata "waathirika wengine", hata hivyo ametangaza Benoît Payan, meya wa mji wa Marseille, Jumatatu asubuhi Aprili 10.

Maafisa wa kikosi cha Zima moto na waokoaji wakiwa katika eneo la tukio ambako nnyumba ya ghorofa nne iliporomoka katika mtaa wa Tivoli huko Marseille, Aprili 10, 2023.
Maafisa wa kikosi cha Zima moto na waokoaji wakiwa katika eneo la tukio ambako nnyumba ya ghorofa nne iliporomoka katika mtaa wa Tivoli huko Marseille, Aprili 10, 2023. © AFP/Nicolas Tucat
Matangazo ya kibiashara

Mtu ambaye alifikiriwa kutoweka katika jengo lililo karibu na lile lililoanguka ghafla katikati mwa Marseille siku ya Jumapili "alijitokeza na ndugu zake", ametangaza, Jumatatu, Aprili 10, mwendesha mashtaka katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.

Kulingana na chanzo hicho, "mwili wa mtu watatu ulitolewa chini ya vifusi". Hapo awali, "maiti mbili" zilipatikana usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu chini ya vifusi vya jengo lililoporomoka kutokana na mlipuko huko Marseille, kikosi cha Zima moto kimetangaza. "Kutokana na matatizo ya kazi ya uokoaji, operesheni ya kutoa miili kwenye eneo la tukio itachukua muda", kikosi cha Zima moto kimebainisha katika taarifa fupi, na kuthibitisha taarifa kutoka La Provence na kituo cha habari cha BFMTV. "Mamlaka ya mahakama kisha itaendelea na zoezi la kutambua miili ya wahanga", taarifa hiyo imeongeza.

Ugunduzi huu unakuja zaidi ya saa 24 baada ya mlipuko mkubwa uliolipua jengo la ghorofa nne huko Marseille. Mwendesha mashtaka wa umma wa Marseille alidokeza mapema Jumapili kwamba wahudumu wa uokoaji bado walikuwa wakiwatafuta watu wanane wanaodhaniwa kupotea kwenye vifusi. Kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka kwa upande wa mashtaka, watu watano bado wamefukiwa chini ya vifusi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.