Pata taarifa kuu

NATO yatoa wito wa kuachiwa huru kwa mwanahabari wa Marekani Evan Gershkovich

Nairobi – Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg hii leo ametaka mamlaka ya Urusi kumuachia mara moja  mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, ambaye amezuiliwa nchini humo kwa tuhuma za ujasusi.

Jens Stoltenberg  ataka mamlaka ya Urusi kumuachia huru  mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich,
Jens Stoltenberg ataka mamlaka ya Urusi kumuachia huru mwandishi wa habari wa Marekani Evan Gershkovich, Kenzo TRIBOUILLARD / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mamlaka ya Urusi walimzuilia mwandishi wa habari wa Marekani wa jarida la Wall Street Journal ,Evan Gershkovich,na kumshutumu kwa madai ya  ujasusi, na hivyo kuashiria kurekebishwa kwa mvutano kati ya Moscow na Marekani na kampeni yake dhidi ya vyombo vya habari vya kigeni, ambayo imekuwa chini ya shinikizo kubwa tangu Rais Vladimir Putin kuzindua taarifa yake kamili. 

"Kukamatwa kwake kunatia wasiwasi mkubwa. Ni muhimu kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari, haki za waandishi wa habari na haki ya kuuliza maswali na kufanya kazi zao," alisema Jens Stoltenberg .

Mkuu huyo aliongeza kuwa anatazamia suala la kuzuiliwa kwa ripota wa Wall Street Journal kuzingatiwa na mawaziri wa mambo ya nje wa NATO katika mkutano wao utakaofanyika hapo kesho jijini Brussels.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atakuwa Brussels vilevile  kukutana na wenzake 29 wa NATO na kuikaribisha Finland kama mwanachama wa 31 wa muungano huo.

Gershkovich, raia wa Marekani mwenye umri wa miaka 31,  naaminika kuwa mwandishi wa habari wa kwanza wa kigeni kushikiliwa kwa ujasusi katika Urusi ya baada ya Soviet.

Mwajiri wake ametupilia mbali madai kwamba alikuwa akijishughulisha na ujasusi, na Blinken tayari amedai kuachiliwa kwake katika wito kwa waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.

uhusiano baina ya Urusi na Marekani unaoenekana kuwa mabya mbaya zaidi baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.