Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Uingereza: Charles III akaribishwa kwa vificho na nderemo alipowasili Ujerumani

Mfalme Charles III amewasili Berlin kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi katika nafasi yake mpya kama mfalme. Akiwa ameandamana na mke wake Camilla, amekaribishwa katika mji mkuu wa Ujerumani na Rais Frank-Walter Steinmeier, wakati wa sherehe maalum mbele ya lango la Brandenburg, katikati mwa mji mkuu.

Mfalme Charles III na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier mbele ya Lango la Brandenburg huko Berlin, Machi 29, 2023.
Mfalme Charles III na Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier mbele ya Lango la Brandenburg huko Berlin, Machi 29, 2023. © AP/Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Berlin, Delphine Nerbollier

Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu wa nchi kupokea heshima za kijeshi mbele ya lango la Brandenburg. Na Charles III ndiye aliyekuwa wa kwanza kupokea heshima hii.

Kwa hafla hiyo, watu 1,500 wameruhusiwa kuhudhuria hafla hii fupi. Wengine hawakubahatika; mamia kadhaa ya watu walikusanyika kando ya barabara inayoelekea lango la Brandenburg kujaribu kuwaona Mfalme Charles III na mkewe kwenye gari lao.

Sherehe hii ya kijeshi iliyosimamiwa na zaidi ya maafisa wa polisi 900 inaashiria mwanzo wa siku tatu za ziara rasmi, katika nchi ambayo Mfalme Charles III anaifahamu vyema. Ikiwa alikuja Ujerumani mara thelathini, hii ni ziara yake ya kwanza kama mfalme.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.