Pata taarifa kuu

Ufaransa: Waandamanaji wakabiliana tena na polisi

NAIROBI – Nchini Ufaransa waandamanaji walikabiliana tena na maafisa wa polisi hapo jana Jumatatu, kuendelea kupinga mageuzi ya mfumo ya pensheni,unaoungwa mkono na rais Emmanuel Macron.

Waandamanaji wamekabiliana na maofisa wa polisi nchini Ufaransa kwa mara nyengine tena
Waandamanaji wamekabiliana na maofisa wa polisi nchini Ufaransa kwa mara nyengine tena AP - Jeremias Gonzalez
Matangazo ya kibiashara

Maelfu ya waandamanaji walijitokeza katika miji mbalimbali nchini humo, kupinga mabadiliko hayo, yanayotaka umri wa wafanyakazi kustaafu uongezwe kutoka miaka 62 hadi 64.

Mashariki mwa jiji la Paris, polisi walitumia vitoa machozi kuwasambaratisa waandamanaji, huku wengine wakikamatwa, baada ya kuzuka kwa vurugu.

Katika mji wa Lyon, vurugu pia zilizuka huku waandamanaji wenye hasira wakivamia kituo cha mabasi, na kusambaratisha shughuli za usafiri.

Rais Macron licha ya kukutana na Waziri Mkuu Elisabeth Borne na Mawaziri katika Ikulu ya Elysee kuwa, mabadiliko hayo yatatekelezwa na hakuna kinachobadilisha mawazo yake, licha ya kuendelea kwa maandamano hayo.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Borne ameomba mazungumzo na viongozi wa vyama vya wafanyazi Jumaatu au Jumanne wiki ijayo, kujadili kinachoendea, wakati huu maandamano na mgomo mwingine ukipangwa tarehe 6 Aprili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.