Pata taarifa kuu

Tuhuma za kukwepa kulipa ushuru: Misako mikubwa yafanyika katika benki tano nchini Ufaransa

'Operesheni kubwa zaidi katika historia ya PNF': Ofisi ya mashtaka ya kifedha imefanya upekuzi mkubwa siku ya Jumanne kulenga benki kuu tano nchini Ufaransa, zinazoshukiwa kutumia mpango wa ushuru wa gawio unaoitwa 'CumCum', ambao unaweza kugharimu zaidi ya euro bilioni moja kwa mamlaka ya ushuru.

Tangu Mei 16, 2018, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kifedha inapatikana ghorofa ya 20 katika jengo la Mahakama ya Paris.
Tangu Mei 16, 2018, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Kifedha inapatikana ghorofa ya 20 katika jengo la Mahakama ya Paris. © Tribunal judiciaire de Paris
Matangazo ya kibiashara

Ni operesheni ya kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, kulingana na chanzo kinachofahamu faili hiyo, iliyofanywa Jumanne asubuhi huko Paris na huko La Défense (Hauts-de-Seine), mahakimu 16 (kati ya 19 wanaohudumu) wa PNF, wachunguzi 150 (kati ya zaidi ya 250 wanaohudumu) kutoka idara ya uchunguzi wa mahakama ya kifedha (SEJF), pamoja na waendesha mashtaka sita wa Ujerumani kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma ya Cologne.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, PNF imethibitisha Jumanne asubuhi habari hii kutoka kwa gazeti la Le Monde ambayo imesema taasisi tano za benki na kifedha zinazopatikana mjini Paris na huko La Défense zinalengwa na opereseni hii. Benki hizo ni pamoja na BNP Paribas, Exane (msimamizi wa hazina, kampuni tanzu ya BNP), Société Générale, Natixis na HSBC, kulingana na chanzo kinachofahamu faili hiyo.

Benki mbili za kwanza zinachunguzwa na PNF kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi na ufujaji wa ukwepaji uliokithiri wa kodi, baada ya ripoti kutoka kwa mamlaka ya kodi. Benki zingine tatu zinachunguzwa kwa ufujaji wa pesa uliokithiri na kukwepa kulipa kodi. Uchunguzi huu wote ulifunguliwa katikati ya mwezi Desemba 2021, kulingana na PNF.

Msemaji wa Societe Generale amelithibitishia shirika la habari la AFP kwamba msako umekuwa ukiendelea katika makao makuu ya benki hiyo tangu Jumanne asubuhi, bila kujua lengo lilikuwa nini. Benki ya Exane imejizuia kusema, wakati benki zingine hazikujibu shirika la habari la AFP. Kwenye Twitter, Waziri wa Hesabu za Umma Gabriel Attal amebaini kwamba "ukaguzi mkubwa" umefanywa na SEJF, ambayo inapanga kutangaza "hivi karibuni uimarishaji mkubwa" kama sehemu ya mpango wake wa kupambana na ukwepaji kodi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.