Pata taarifa kuu

Uturuki: Kemal Kiliçdaroglu ateuliwa kuwa mgombea wa upinzani dhidi ya Erdogan

Muungano wa vyama sita vya upinzani vya Uturuki umemteua Jumatatu hii, Machi 6 Kemal Kiliçdaroglu, kiongozi wa muundo wake mkuu, kukabiliana na mkuu wa nchi Recep Tayyip Erdogan, madarakani kwa miaka ishirini, katika uchaguzi wa urais wa Mei 14.

Kemal Kiliçdaroglu, 74, ameongoza chama cha Republican People's Party tangu 2010.
Kemal Kiliçdaroglu, 74, ameongoza chama cha Republican People's Party tangu 2010. AFP - ADEM ALTAN
Matangazo ya kibiashara

Siku tatu baada ya kukaribia kuvunjika, muungano wa upinzani hatimaye ulipata mgombea wake katika uchaguzi wa urais. Wakiwa wamekusanyika katika makao makuu ya Chama cha Felicity huko Ankara, viongozi wa vyama sita vya upinzani vinavyounda muungano huu wamemteua Kemal Kiliçdaroglu kukabiliana na Recep Tayyip Erdogan katika uchaguzi wa urais wa mwezi Mei.

Kemal Kiliçdaroglu, mkuu wa Chama cha Republican People's Party (CHP, social democrat) tangu 2010, ameahidi kurejea kwenye mchezo wa kidemokrasia iwapo atachaguliwa. "Sote kwa pamoja tutaweka nguvu ya maadili na haki," amesema katika tangazo hilo. "Sisi, kama Muungano wa Kitaifa, tutaongoza Uturuki kwa kuzingatia mashauriano na maelewano," ameongeza.

Rais wa Chama cha Good Party (mzalendo), chama cha pili muhimu katika muungano huo, alipinga vikali kugombea kwake, akiwataka mameya maarufu wa CHP wa Istanbul na Ankara, Ekrem Imamoglu na Mansur Yavas, kugombea nafasi yake - hata hivyo walikataa. Baada ya kukutana na mameya hao wawili na kisha Kemal Kiliçdaroglu mjini Ankara siku ya Jumatatu, kiongozi wa Chama cha Good Party, Meral Aksener, hatimaye amerejea tena kwenye nafasi yake kwenye meza ya Muungano.

Uchaguzi unaotia wasiwasi

Kwa baadhi ya wafuasi wa upinzani, Kemal Kiliçdaroglu, afisa mwandamizi wa zamani mwenye umri wa miaka 74 kutoka wachache wa Alevi, anakumbwa na ukosefu wa hisani mbele ya mkuu wa nchi anaye maliza muda wake, atatetea kiti chake. Lakini Recep Tayyip Erdogan, ambaye umaarufu wake umekumbwa na mzozo wa kiuchumi ambao Uturuki inaendelea kupitia, atalazimika kujibu kwa wapiga kura kwa ucheleweshaji wa misaada katika saa kufuatia tetemeko la ardhi la Februari 6. Mapungufu ambayo mpinzani wake mteule hakukosa kuyataja, akikemea “uzembe” na ufisadi katika uongozi wa nchi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.