Pata taarifa kuu

Biden aendelea kuikosoa Urusi kujiondoa kwa mkataba wa nyuklia

NAIROBI – Rais wa Marekani, Joe Biden, ameikosoa Urusi baada ya kutangaza kujitoa kwenye mkataba wa nyuklia kati ya nchi hizo mbili uliokuwa umetiwa saini mwaka 2010, hata akisema haoni Moscow ikitumia silaha hizo.

Rais wa Marekani Joe Biden na Vladimir Putin  wa Urusi
Rais wa Marekani Joe Biden na Vladimir Putin wa Urusi © Reuters/Kevin Lamarque - Sputnik/Iliya Pitalev - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, rais Biden, ameahidi nchi yake kulinda kila kona ya nchi mwanachama wa jumuiya ya NATO.

“Msimamo wa Marekani kwa washirika wa NATO nilishawahi kuusema na nitausema tena kwamba uko wazi kabisa, ibara ya tano ni siri ambayo Marekani iliweka msimamo.”ameeleza rais Joe Biden.

Hata hivyo, Urusi licha ya kujitoa kwenye mkataba wa New START, imesema haina mpango wa kutumia silaha hizo hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.