Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Ufaransa: Mwalimu auawa kwa kisu na mwanafunzi Saint-Jean-de-Luz

Mwalimu kutoka shule ya kibinafsi huko Saint-Jean-de Luz (Pyrénées-Atlantiques) amefariki baada ya kudungwa kisu na mwanafunzi siku ya Jumatano, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Bayonne.

Gari la polisi.
Gari la polisi. AP - Francois Mori
Matangazo ya kibiashara

"Ninaweza kuthibitisha kwamba kweli kulikuwa na shambulio la kisu na kwamba mwathiriwa amefariki dunia," mwendesha mashtaka Jérôme Bourrier ameliambia shirika la habari la AFP. Mwanafunzi huyo amekamatwa, kikosi cha Zima moto kimesema.Tukio hilo limetokea katika shule ya upili ya Saint-Thomas d'Aquin huko Saint-Jean-de-Luz.

Kulingana na tovuti ya habari ya Actu.fr katika Nchi ya Basque, ambayo ilifichua habari hiyo, mhanga alikuwa na umri wa miaka 52.

Kulingana na gazeti la Sud Ouest, ni mwalimu Mhispania aliyekuwa akitoa kozi kwa darasa la pili. Mhusika wa shambulio hilo mbaya aliingia na kisu darasani na kumshambulia kikatili mwalimu huyo.

Kwa hofu, wanafunzi darasani walikimbia kupitia mlango unaoelekea kwenye darasa lingine. Kulingana na vyombo vingine vya habari, mshambulizi huyo aliripotiwa kusema "alimilikiwa" na alisikia sauti. Mbali na mazingira ya tukio, uchunguzi utaamua hali ya kisaikolojia na sababu za mwanafunzi huyu.

Waziri wa Elimu awasili katika eneo la tukio

Saa sita mchana, wanafunzi walikuwa wakitoka shuleni taratibu baada ya kufungiwa kwenye madarasa yao kwa takriban saa mbili na kuungana na wazazi wao nyuma ya lango la shule hii ya katikati mwa jiji yenye wanafunzi wapatao 1,100, ameshuhudia mwandishi wa shirika la habari la AFP. Ni wazazi wa wanafunzi wa darasa husika tu ndio waliweza kuingia katika eneo la shule.

Hii ni mara ya kwanza kwa mwalimu kuuawa kama sehemu ya kazi yake nchini Ufaransa tangu kuuawa kwa Samuel Paty mnamo 2020 huko Val-d'Oise. Mnamo mwezi Julai 2014, mwalimu mwenye umri wa miaka 34 aliuawa kwa kuchomwa kisu na mama wa mwanafunzi katika shule moja huko Albi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.