Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Kesi ya ubakaji ya Saad Lamjarred yafunguliwa mjini Paris

Kesi ya mwanamuzi nguli wa Morocco Saad Lamjarred, anayeshtakiwa kwa kumbaka na kumpiga msichana mmoja katika chumba cha hoteli mnamo mwaka 2016 kando ya tamasha iliyopangwa huko Paris, imefunguliwa leo Jumatatu asubuhi katika mji mkuu wa Ufaransa.

Mwanamuziki nguli wa Morocco Saad Lamjarred mnamo Julai 30, 2016 kwenye Tamasha la Kimataifa la Carthage, karibu na Tunis. Kesi yake ya ubakaji uliokithiri imeanza Februari 20, 2023 katika Mahakama ya Paris.
Mwanamuziki nguli wa Morocco Saad Lamjarred mnamo Julai 30, 2016 kwenye Tamasha la Kimataifa la Carthage, karibu na Tunis. Kesi yake ya ubakaji uliokithiri imeanza Februari 20, 2023 katika Mahakama ya Paris. AFP - FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Saad Lamjarred, ambaye sasa ana umri wa miaka 37, ameripoti mbele ya Mahakama ya Paris. Akiwa amevaliasuti nyeusi na shati jeupe, alichukua nafasi yake katika safu ya mbele, sambamba na mkalimani. Laura P., mlalamikaji, alimtazama na kuanza kuangusha kilio.

Saad Lamjarred aliposimama kueleza utambulisho na taaluma yake, 'msanii', kizimani, mlalamikaji aligeuza kichwa chake, akitazama chini.

Mambo ambayo anashutumu yalianza Oktoba 2016. Akiwa na umri wa miaka 20, alimfuata mwanamuziki nguli huyo na marafiki zake kadhaa kwenye "sherehe" baada ya kukutana nao katika klabu ya usiku. Jioni aliandamana na Saad Lamjarred hadi hotelini kwake katika mtaa wa Champs Élysées.

Walibusana lakini alipozidi kustaajabisha, alijaribu kumzuia, mlalamikaji aliwaambia wachunguzi. "Kisha nilipiwa na kubakwa, " alisema. Alitoroka chumbani na alisaidiwa na wafanyakazi wa hoteli, ambao walielezea "mwanamke aliyetishwa" na kulia. Wafanyakazi hawa walimzuia mtu ambaye alidaiwa kuwa mlevi aliyekuwa akimkimbiza.

Saad Lamjarred anadai kuwa alijitetea tu wakati Laura P. alipomvamia ghafla walipokuwa wakibusana, na kupinga unyanyasaji wowote. Alimshitaki tu ili kuepuka "kashfa" kwa sababu alikuwa anajulikana. Mwanamuziki huyo, anayependwa nchini Morocco na maarufu katika ulimwengu wote wa Kiarabu, alikuwa Paris kwa tamasha lililopangwa katika mji mkuu.

Akiwa amefungwa katika mchakato huo, aliachiliwa chini ya bangili ya kielektroniki mnamo 2017 - kabla ya kuzuiliwa kwa muda mfupi tena mnamo 2018 kwa sababu alishtakiwa kwa ubakaji wa msichana mwingine huko Saint-Tropez, Côte d' Azur (kusini-mashariki mwa Ufaransa) .

Saad Lamjarred pia alihusishwa na ubakaji katika mazingira kama hayo huko Casablanca na New York. Kesi yake mjini Paris itasikilizwa hadi siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.