Pata taarifa kuu

Scotland: Waziri wa mkuu Nicola Sturgeon atangaza kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Scotland Nicola Sturgeon ametangaza Jumatano Februari 15 kujiuzulu kwenye wadhifa wake baada ya miaka minane madarakani, huku akiacha maswali nyuma yake kuanzia mrithi wa kiti hicho hadi suala la uhuru wa Scotland ambalo  bado halijapatiwa ufumbuzi.

Nicola Sturgeon, Waziri mkuu wa Scotland, ametangaza kujiuzulu Jumanne Februari 15, 2022.
Nicola Sturgeon, Waziri mkuu wa Scotland, ametangaza kujiuzulu Jumanne Februari 15, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

"Sikuzote nimezingatia kwamba kutumika vyema ni kuona wakati unapowadia kutoa nafasi kwa ajili ya mtu mwingine," amesema Waziri mkuu wa Scotland. Nicola Sturgeon anaona kuwa wakati wa kujiuzulu umefika, kwa chama chake, kwa taifa lake, Scotland, na yeye mwenyewe.

"Kazi hii, anasema, ni fursa kubwa, lakini pia ngumu sana. Siwezi tena kuipa kazi yangu nguvu inayostahili”.

Uamuzi huu pia unatokana na itikadi kali za mjadala katika miaka ya hivi karibuni. Lakini kuondoka huku, anaelezea Waziri mkuu wa Scotland, hakuhusiani kwa namna yoyote na masuala yaliyojitokeza hivi karibuni, bali anauchukua baada ya kujitathmini kwa muda mrefu. Akikosolewa na wabunge wa chama chake mjini London, alishindwa kuendeleza kwa kiasi kikubwa suala la uhuru wa Scotland katika kipindi cha miaka minane madarakani.

Kiwango chake cha umaarufu kimekuwa kikishuka tangu mwezi Desemba, kwa sehemu kwa sababu ya maoni yake juu ya haki za watu waliobadili jinsia. Hata hivyo, kujiuzulu huku kulishangaza kila mtu, huko London na Edinburgh, ambaye alitarajia kujiondoa kwenye nafasi ya kiongozi wa chama cha SNP katika uchaguzi ujao, mnamo 2025.

Scotland ni moja ya nchi nne zenye mamlaka ya ndani ambazo zinaunda taifa la Uingereza, nyingine zikiwa England, Wales na Ireland Kaskazini.

Nicola Sturgeon atasalia madarakani hadi kuchaguliwa kwa kiongozi mpya wa chama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.