Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Ufaransa: Vyama vya wafanyakazi vyaendelea kupinga mradi wa serikali kuhusu pensheni

Kutoka Arras hadi Nice, wapinzani wa mageuzi ya pensheni wanaandamana ambapo Jumanne hii, mamia kwa maelfu ya watu wa Ufaransa wanatarajiwa kuingia mitaani, vyama vya wafanyakazi vinatarajia uhamasishaji angalau sawa na ule wa Januari 19 ili kuifanya serikali kusitisha mradi wake muhimu.

Wakati wa maandamano huko Marseille mnamo Januari 31, 2023.
Wakati wa maandamano huko Marseille mnamo Januari 31, 2023. AFP - CHRISTOPHE SIMON
Matangazo ya kibiashara

Takriban waandamanaji milioni 1.2 wanatarajiwa kuingia mitaani, ikiwa ni pamoja na 100,000 huko Paris, kulingana na polisi. Kwa jumla, zaidi ya maandamano 200 dhidi ya mageuzi ya pensheni yamepangwa kufanyika Jumanne kote nchini Ufaransa.

Kiongozi wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, CFDT, Laurent Berger amesema kuwa kumekuwa na "watu wengi" mitaani kuliko siku ya mwisho ya uhamasishaji. "Ripoti mbalimbali ambazo zinatufiki kutoka kote nchini, zinabaini kwamba watu ni wengi mitaani kuliko Januari 19," amesema Bw. Berger, wakati mwenzake wa muungano wa CGT Philippe Martinez akibaini kwamba waandamanaji "angalau ni wengi".

Kote Ufaransa, maandamano ya kwanza yalianza saa nne kamili wakipinga mageuzi kabambe ya Emmanuel Macron ya kusogeza mbele umri wa kisheria wa kustaafu hadi miaka 64, hasa kwa wanawake, na kwa mfano huko Toulouse kundi la watetezi wa haki za wanawake linaongoza maandamano hayo.

Takwimu za kwanza zilikuwa katika idadi sawa na zile za 19 na, kwa mfano, 14,000 huko Rouen (ikilinganishwa na 13,000) na 12,000 huko Le Havre (ikilinganishwa na 11,000). Kwa mara nyingine tena, miji yenye ukubwa wa kati ilionekana kuwa mstari wa mbele ikiwa na waandamanaji 7,000, kama tarehe 19, huko Alès au 8,500 huko Angoulême (9,000 tarehe 19)

Katika Reunion, zaidi ya watu 10,000 kulingana na waandaaji, 7,300 kulingana na Halmashauri ya mkoa, wameandamana katika miji miwili mikubwa ya kisiwa hicho.

Huko Paris, maandamano yalianza saa 2:15 (nane na dakika kumi na tano) kutoka Place d'Italie, yakiongozwa na viongozi wa vyama vya umoja (CFDT, CGT, FO, CFE-CGC, CFTC, Unsa, Solidaires, FSU) walikusanyika nyuma ya mabango yaliyo andikwa " marekebisho ya pensheni: kufanya kazi kwa muda mrefu ni hapana "ambayo tayari walikuwa wakionyesha mnamo Januari 19.

Polisi na askari elfu kumi na moja wamemewekwa tayari, wakiwemo 4,000 mjini Paris, kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin.

Muungano baina ya vyama vya wafanyakazi watakutana kuanzia saa kumi na mbili (6:00) jioni katika makao makuu ya FO ili kuamua juu ya ufuatiliaji wa maandamani, na pengine kutangaza angalau siku mpya ya maandamano.

Sekta nyingi kwenye mgomo

Shule zimefungwa, treni, mabasi au metro ambazo hazipiti, upotezaji wa nguvu kwenye mtandao wa umeme na usafirishaji umezuiwa katika vituo vya kusafisha: sekta nyingi zimesitisha kazi Jumanne ili kuonyesha kupinga mageuzi ya pensheni.

Kiwango cha walimu waliogoma ni 25.92%, ikijumuisha 26.65% ya shule za msingi na 25.22% shule za sekondari (shule za kati na sekondari) kulingana na wizara, chini ya takwimu za vyama. Mnamo Januari 19, katika siku ya kwanza ya uhamasishaji, kiwango cha walimu waliogoma kilikuwa 42.35% katika elimu ya msingi na 34.66% katika elimu ya sekondari, kulingana na wizara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.