UJERUMANI- UFARANSA-USHIRIKIANO
Ufaransa na Ujuerumani kuimarisha uhusiano wao
Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz na rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, wamekubaliana kuimarisha uhusiano wa nchi zao, licha ya mvutano uliosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Cheza - 00:52
Matangazo ya kibiashara
Katika hotuba yake rais Macron, amesema kuna mambo mengi ya muhimu kwa nchik hizo kushirikiana kuliko tofauti walizonazo.
“Ujerumani na Ufaransa kwa sababu tayari zimesha safisha njia ya upatanisho lazima wawe waanzilishi wakuijenga upya ulaya yetu.”amesema rais Macron.
Juma lililopita Ufaransa haikufurahishwa na Ujerumani, baada ya kukataa kutoa msaada wa vifauri vyake vya kisasa kwa Ukraine.