Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UFARANSA- USHIRIKIANO

Ufaransa inasubiri maelezo ya kina kutoka Bamako baada kutakiwa kuwaondoa wanajeshi

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, hapo jana amesema nchi yake inasubiri maelezo ya kina kutoka kwa Serikali ya Burkina Faso, baada ya kutoa mwezi mmoja kwa wanajeshi wake kuondoka nchini humo.Mwandishi wetu Reuben Lukumbuka na maelezo zaidi

 Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa
Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Rais Macron, amewaambia waandishi wa habari kuwa serikali yake inasubiri maelezo ya kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Ibrahim Traore, kuhusu sababu za kufikia uamuzi huo.

Hata hivyo taarifa za kidiplomasia kutoka ndani ya Serikali ya Ouagadogou, zinasema hatua hiyo haina nia ya kuzorotesha uhusiano wa nchi hizo, lakini inahusiana na mktaba wa ushirikiano wa kijeshi waliotiliana saini.

Uamuzi huu wa Burkina Faso, unafanana na ume uliochukuliwa na Serikali ya Mali, ambayo nayo iliwafurusha wanajeshi wa Ufaransa kwa madai ya kuwasaidia wanajihadi wa kiislamu.

Ufaransa ina jumla ya wanajeshi 400 wa kikosi chake maalum nchini Burkina Faso.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.