Pata taarifa kuu

Katibu Mkuu wa NATO aahidi silaha nzito zaidi kwa Ukraine 'katika siku za usoni'

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema Jumapili hii, Januari 15, 2023 katika mahojiano na vyombo vya habari vya Ujerumani Handelsblatt kwamba Ukraine inaweza kutarajia uwasilishaji mpya wa silaha nzito kutoka kwa washirika wake wa Magharibi.

Jens Stoltenberg amehakikisha kwamba vita na Urusi vinaingia katika "hatua yenye maamuzi" na kwamba ni muhimu kuipa Ukraine "silaha inayohitaji ili kushinda vita vyake dhidi ya Urusi".
Jens Stoltenberg amehakikisha kwamba vita na Urusi vinaingia katika "hatua yenye maamuzi" na kwamba ni muhimu kuipa Ukraine "silaha inayohitaji ili kushinda vita vyake dhidi ya Urusi". © Alexandru Dobre / AP
Matangazo ya kibiashara

"NATO itaendelea kuiunga mkono Ukraine kijeshi, " amesema Jens Stoltenberg, huku akihakikisha kwamba jeshi la Ukraine hivi karibuni litapokea silaha mpya nzito kutoka kwa washirika wake wa Magharibi. 

"Ahadi za hivi karibuni za silaha nzito ni muhimu - na ninatarajia kutakuwa na zaidi katika siku za usoni," Jens Stoltenberg amesema kabla ya mkutano mwingine wa Januari 20 wa uratibu wa mataifa ya Magharibi kuleta msaada kwa Ukraine, katika kambi ya Marekani huko Ramstein, nchini Ujerumani.

Pia amehakikisha kwamba vita na Urusi vinaingia katika "hatua yenye maamuzi" na kwamba ni muhimu kuipa Ukraine "silaha inayohitaji ili kushinda vita vyake dhidi ya Urusi". 

Mabadiliko ya mkakati

Wakati wa miezi ya kwanza ya mzozo huo, washirika wa Magharibi wa Ukraine walisitasita kuwasilisha silaha nzito kwa Ukraine, hasa kwa sababu ya hali ambayo ingeweza kuzuka nchini Urusi.

Hata hivyo, Ufaransa, Ujerumani na Marekani sasa wamebadilisha utaraibu. Kyiv inatarajia kupokea magari ya kivita yenye ubora na nguvu zaidi. Uingereza pia hivi majuzi ilibaini kuwa itatoa vifaru vipy aina ya Challenger 2 na mifumo ya ulinzi kwa Ukraine, na kuwa nchi ya kwanza kusambaza vifaru vizito kutoka nchi za Magharibi kwa Kyiv.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.