Pata taarifa kuu
VATICAN- MAOMBOLEZO

Zoezi la kuutazama mwili wa Papa Benedict wa 16 imeanza mjini Vatican

Maelfu wa waumini wa kanisa Katoliki, mapema Jumatatu wametoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi wao wa zamani Papa Benedict wa 16 mjini Vatican.

Waumini wa kanisa Katoliki wakisubiri kuutazama mwili wa Papa Benedict wa 16
Waumini wa kanisa Katoliki wakisubiri kuutazama mwili wa Papa Benedict wa 16 AFP - TIZIANA FABI
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kuutazama mwili wa Papa huyo wa zamani limeratibiwa kufanyika kwa kipindi cha siku tatu kwanzia leo Jumatatu katika kanisa la Peter's Basilica kabala ya mazishi yake.

Papa Benedict, aliongoza kanisa Katoliki kwa kipindi cha miaka minane ambapo alikuwa  kiongozi wa kwanza katika kipindi cha miaka 600 kujiuzulu kwa kile alichokisema ni kwa sababu ya umri wake mkubwa na kuanza kudhoofika kwa afya yake.

Mwezi uliopita Papa Francis aliweka wazi kwamba alisaini barua alipoingia uongozini kwamba atajiuzulu iwapo afya yake haitamruhusu kutekeleza majukumu yake.

Mrithi wake Papa Francis, anatarajiwa kuongoza ibaada ya maziko yake alhamisi wiki hii.

Vatican haijatoa orodha kuhusu wageni watakaohudhuria ibaada ya wafu japokuwa imesema itawajumuisha wajumbe kutoka nchini Italia pamoja wageni kutoka nchini Ujerumani aliko zaliwa kiongozi huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.