Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA

Brazil: Rais mpya Lula da Silva ameahidi kujenga taifa upya baada yake kuapishwa

Luiz Inacio Lula da Silva, ameapishwa kuongoza nchi ya Brazil kwa mara nyingine ambapo ameahidi kujenga upya nchi hiyo  iliyoshuhudiwa mgawanyiko mkubwa wa kisiasa wakati wa utawala wa kiongozi wa zamani Jair Bolsonaro .

Rais mpya wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakati akila kiapo cha kuongoza nchi.
Rais mpya wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakati akila kiapo cha kuongoza nchi. © REUTERS/Adriano Machado
Matangazo ya kibiashara

Lula da Silva, mwenye umri wa miaka 77 ,amekula kiapo  kwenye sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu  na kususiwa na mtangulizi wake Bolsonaro, kinyume na tamaduni za nchi hiyo,ambapo kiongozi mpya hukabidhiwa joho la njano na kijani na mtangulizi wake.

Ameahidi kupigania watu wa mapato ya chini ,kupigana na ubaguzi  na ukataji miti kwenye msitu wa Amazon ,uliozidi wakati wa utawala wa Bolsonaro.

Amewaomba raia wa Brazil ambao hawakuumuunga mkono kwa kumpigia kura, kuungana naye katika ujenzi wa taifa akisema raia wa Brazil ni kitu kimoja.

Lu da Silva aliwahi kuongoza nchi hiyo mwaka 2003 hadi 2010, kabla kukabiliwa na kesi ya ufisadi ambapo alilazimika kukaa jela kwa miaka mitano kesi hiyo ikitupwa baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.