Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Mashambulio ya jeshi la Urusi, yamesabisha majeraha ya watu watatu Ukraine

Ukraine inasema, miji yake kote nchini imekuwa ikishambuliwa na makombora ya Urusi, ikiwa ni mojawapo ya mashambulio makubwa tangu kuvamiwa kwa nchi yake mwezi Februari.

Makazi yalioharibiwa na Makombora ya Urusi nchini Ukraine
Makazi yalioharibiwa na Makombora ya Urusi nchini Ukraine © 路透社图片
Matangazo ya kibiashara

Meya wa jiji kuu Kyiev, Vitaliy Klitschko, amesema mashambulio ya jeshi la Urusi, yamesabisha majeraha ya watu watatu, akiwemo msichana mwenye umri wa miaka 14.

Mbali na Kiev, mashambulio ya makombora, yameshuhuduwa katika miji mingine ya Kharkiv, Odesa , Lviv miongoni mwa mingine.

Aidha, mashambulio la Kyiv yamewaacha asilimia 40 ya wakaazi, wakisalia bila umeme.

Nalo Jeshi la Ukraine linasema, makombora 69 yamerushwa nchini humo, huku ikifanikiwa kuzuia makombora 54.

Awali, msemaji wa rais Mykhailo Podolyak, alisema makombora 120 yalikuwa yamerushwa kulenga maeneo wanakoishi raia.

Katika hatua nyingine, nchi ya Belarus imesema, kombora la Ukraine limefika katika ardhi yake, na kuzua wasiwasi wa kusambaa kwa vita hivyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.