Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Ufaransa: Jordan Bardella achaguliwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Rassemblement National

Nchini Ufaransa, chama cha siasa cha mrengo wa kulia Rassemblement National (RN), kimemchagua Jordan Bardella kuwa kiongozi mpya wa chama hicho kuchukua nafasi ya mwanasiasa mkongwe Marine Le Pen.

Kiongozi mpya wa chama cha Rassemblement National (RN), Jordan Bardella
Kiongozi mpya wa chama cha Rassemblement National (RN), Jordan Bardella REUTERS - CHRISTIAN HARTMANN
Matangazo ya kibiashara

Bardella mwenye umri wa miaka 27, amepata uungwaji mkubwa, baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa mwaka mmoja.

Baada ya kupigwa kura, mwanasiasa huyo kijana, anayeelezwa mzalendo wa chama hicho, alipata asilimia 85 ya kura huku mpinzani wake, Louis Aliot akipata asilimia 15.

Hii ndio mara ya Kwanza kwa chama hicho kuongozwa na mtu, asiyetoka katika família ya Le Pen.

Chama hiki, zamani kilifahamika kama Front Nationale chenye sera ya kupinga wahamiaji na kutounga mkono baadhi ya sera za umoja wa Ulaya, kilianzishwa na baba yake Marine, Jean-Marie Le Pen mwaka 1972.

Marine Le Pen alitangaza kujiondoa kwenye uongozi wa chama hicho mwaka 2021 kuelekea uchaguzi wa urais mwaka huu, na kuwa mpinzani mkuu wa rais Emmanuel Macron, aliyemshinda.

Marine ambaye anatarajiwa kuwania tena urais mwaka 2027, amesema kuondoka kwake hakumaanisha kuwa yuko likizo, huku kiongozi mpya akisema ataeleza jitihada za kuwavutia wapiga kura kutoka mirengo mingine ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.