Pata taarifa kuu

Ajali ya helikopta yaua watu saba kusini mwa Italia

Helikopta iliyokuwa ikiruka kutoka mji wa Foggia, huko Puglia, kwenda Visiwa vya Tremiti, karibu na pwani ya Italia, imekumbana na hali mbaya ya hewa na kuanguka siku ya Jumamosi na kuua watu wote saba waliokuwa ndani. Helikopta hii ambayo imekuwa ikifanya safari ya kila siku, ilitoweka kutoka kwa rada huko Castelpagano di Apricena, eneo la mashambani la Puglia.

Miongoni mwa waliofariki ni familia ya watu wanne kutoka Slovenia, kulingana na Gazeti la Corriere della Sera. Waathiriwa wengine ni daktari wa eneo hilo na marubani wawili wa helikopta hiyo.
Miongoni mwa waliofariki ni familia ya watu wanne kutoka Slovenia, kulingana na Gazeti la Corriere della Sera. Waathiriwa wengine ni daktari wa eneo hilo na marubani wawili wa helikopta hiyo. AFP/Luis Robayo
Matangazo ya kibiashara

Helikopta ilianguka kusini mwa Italia siku ya Jumamosi, na kuua watu wote saba waliokuwa ndani, ikiwa ni pamoja na familia ya watalii wa Slovenia, vyombo vya habari vya Italia vimùeripoti.

Makamu wa rais wa eneo hilo, Raffaele Piemontese, alionyesha kuwa helikopta hiyo ilipatikana ikiwa na watu saba waliokuwa ndani yake, linaripoti gazeti la kila siku la Corriere della Sera. Miongoni mwa wahasiriwa ni familia ya watu wanne kutoka Slovenia, akiwemo msichana wa miaka 13, gazeti hilo lilmema. Waathiriwa wengine ni daktari wa eneo hilo na marubani wawili wa helikopta hiyo.

Meya wa visiwa hivyo, Peppino Calabrese, ameviambia vyombo vya habari kwamba daktari aliamua dakika za mwisho kuchukua helikopta badala ya feri "kutokana na hali mbaya ya baharini". "Jamii yetu iko katika mshtuko. Tukio hili halijawahi kumtokea katika kipindi cha miaka 30  akiwa kazinii,” amesema.

Miongoni mwa waliofariki ni familia ya watu wanne kutoka Slovenia, kulingana na Gazeti la Corriere della Sera. Waathiriwa wengine ni daktari wa eneo hilo na marubani wawili wa helikopta hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.