Pata taarifa kuu

Macron na Scholz waweka pamoja tofauti zao wakati wa mazungumzo 'ya kirafiki' na 'ya kujenga'

Mkutano wa Jumatano hii huko Paris kati ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz umefanyika kwa mazungumzo "ya kirafiki" na "ya kujenga", pande hizo mbili zimetangaza, wakati uhusiano kati ya nchi hizo mbili ukikumbwa na hali ya kutoelewana.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kulia, akimkaribisha Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Jumatano, Oktoba 26, 2022. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana mjini Paris na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani huku kukiwa na tofauti kati ya majirani hao wawili na washirika wakuu wa Umoja wa Ulaya juu ya mkakati wa EU, ulinzi na sera za kiuchumi.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kulia, akimkaribisha Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz katika Ikulu ya Elysee mjini Paris, Jumatano, Oktoba 26, 2022. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekutana mjini Paris na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani huku kukiwa na tofauti kati ya majirani hao wawili na washirika wakuu wa Umoja wa Ulaya juu ya mkakati wa EU, ulinzi na sera za kiuchumi. AP - Christophe Ena
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, ambao umechukua muda wa saa tatu na kumalizika kwa mvutano kati ya Emmanuel Macron na Olaf Scholz, ulifanya iwezekane kujadili "mitazamo ambayo Ulaya inataka na itatumia" na itaongoza wiki hizi zijazo kwa ushirikiano 'mkubwa wenye ubora zaidi', kimesema chanzo cha kidiplomasia cha Ujerumani. Kwa upande wake, rais wa Ufaransa pia amekaribisha mazungumzo "ya kujenga sana", wakati ambapo viongozi hao "wamejadili uhusiano kati ya Ufaransa na jerumani kwa ushirikiano mzuri na wa karibu katika muda wa kati na mrefu".

Msemaji wa serikali ya Ufaransa, Olivier Veran amesema ziara ya Kansela Scholz inaonyesha uwezo wa nchi mbili, Ufaransa na Ujerumani kuzikabili tofauti baina yao pale maslahi ya nchi moja yanapogongana na ya nchi nyingine.

Wakati wa mkutano huu, viongozi hao wawili walikubaliana hasa juu ya ukweli kwamba Umoja wa Ulaya unakabiliwa na "moja ya migogoro muhimu zaidi katika historia yake", ambayo ilisababisha kutaja - pamoja na mambo mengine - maswali ya "usalama na ulinzi", suala la"nishati kwa kuangalia bei ya juu ya nishati na usambazaji" au hata uvumbuzi, aameongeza chanzo cha kidiplomasia  cha Ujerumani.

Mada hizi tatu ni vyanzo vya mvutano kati ya miji mikuu miwili, Paris na Berlin kutokuwa na mawazo sawa juu ya njia za kupambana dhidi ya kupanda kwa bei ya nishati, kwa mfano. "Katika mada hizi tatu, vikundi vya kazi vimeanzishwa ambavyo vitaongoza serikali mbili kufanya kazi kwa karibu katika siku zijazo kwa nia ya hatua zinazofuata," Elysée imesema. Viongozi hao wawili pia wamekubaliana kubadilishana "kabla na baada" ziara ijayo ya Kansela wa Ujerumani nchini China na ziara ya rais wa Ufaransa nchini Marekani.

Tofauti kati ya Ujerumani na Ufaransa sio kitu kipya. Nchi hizo zenye uchumi mkubwa zaidi katika Umoja wa Ulaya na zinazotazamwa kama injini ya umoja huo, zimezoea kuwa na mitazamo inayokinzana juu ya usalama, nishati na masuala mengine.

Akizungumza mjini Brussels wiki iliyopita, Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alisema lengo lake mara zote limekuwa kuimarisha umoja wa Ulaya na mahusiano mema na Ujerumani, na kuongeza kuwa kujitenga kando kwa Ujerumani hakuna tija kwa nchi hiyo wala kwa Ulaya kwa ujumla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.