Pata taarifa kuu

Changamoto za kiuchumi zinazomkabili Waziri Mkuu mpya wa Uingereza

Nchini Uingereza, Rishi Sunak anamrithi Liz Truss kama Waziri Mkuu. Kipaumbele chake cha kwanza kitakuwa kurejesha imani katika uchumi, ulioharibiwa kabisa na serikali zilizopita.

Dharura ya kwanza ya kuchukua nafasi ya Liz Truss itakuwa kurejesha imani katika uchumi wa Uingereza.
Dharura ya kwanza ya kuchukua nafasi ya Liz Truss itakuwa kurejesha imani katika uchumi wa Uingereza. REUTERS - Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Liz Truss, ambaye amekuwa mamlakani kwa muda mfupi zaidi, siku 44, alikuwa mharibifu zaidi kwa mpango wake ambao haukufadhiliwa wa kupunguza kodi kwa matajiri. Masoko yalimfanya alipe uamuzi huu usiofaa katikati ya mgogoro. Na mwishowe, ni Waingereza anaokabiliwa na hali hiyo: mfumuko wa bei kwa 10%, wa juu zaidi katika kundi la nchi tajiri duniani G7 na wa juu zaidi kwa miaka 40, unapunguza nguvu zao za ununuzi. Matumizi yameathiriwa, yalishuka kwa 1.4% mnamo mwezi Septemba. Pauni iko chini kabisa na viwango vya riba vinaongezeka, huku deni likipanda kwa kiwango cha kutisha; deni lina uzito mkubwa kuliko Pato la Taifa la nchi, leo. Mdororo wa uchumi wa Uingereza unatangazwa kwa 2023 na IMF kama wachambuzi wa benki za kibinafsi.

Je, Waziri Mkuu mpya anawezaje kurekebisha hali hiyo?

Jeremy Hunt, Waziri wa Fedha wa muda mfupi aliyeitwa kuokoa hali hiyo na Liz Truss, ameonya: maamuzi magumu yatabidi kufanywa kwa bajeti ijayo. Alidokeza kupunguzwa kwa matumizi ya umma, suluhu pekee la ongezeko la kodi ili kuleta fedha mpya katika hazina ya Serikali inayokabiliwa na gharama ya deni lake ambalo limekuwa kubwa. Chaguo gumu wakati kaya zinahitaji usaidizi wa umma zaidi kuliko hapo awali ili kupitia shida ya nishati. Rishi Sunak, Kansela wa zamani wa Hazina, anafaa kazi hiyo. Yeye ni mlezi wa kanuni za bajeti. Alipokuwa kwenye wadhifa, chini ya uongozi wa Boris Johnson, aliinua kodi wa kampuni na michango ya kijamii, kesho ataweza kuongeza mzigo wa kodi kwa faida kubwa.

Je, matatizo ya sasa ya uchumi wa Uingereza yanahusiana na Brexit?

Janga la Uviko-19 na kisha mzozo wa nishati uliongezeka mara kumi na vita huko Ukraine ndio chanzo chakushuka kwa uchumi wa ingereza. Lakini mishtuko hii hutokea katika uchumi ambao tayari umedhoofishwa na Brexit. Kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya kumezidisha uhaba wa wafanyakazi. Haijabadilisha kushuka kwa tija, kinyume chake imeikuza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.