Pata taarifa kuu

Uingereza: Mfumuko wa bei bado uko juu zaidi, Lizz Truss akosolewa

Mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 10.1 kwa mwaka nchini Uingereza, kiwango cha juu zaidi katika miaka 40 na cha juu zaidi kati ya kundi la nchi 7 zenye uchumi wa juu zaidi duniani, G7, na kuifanya kuwa shida kubwa kwa Benki ya Uingereza na kwa serikali ya Liz Truss.

Mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 10.1 kwa mwaka nchini Uingereza, kiwango cha juu zaidi katika miaka 40 na cha juu zaidi kati ya nchi za G7, na kuifanya kuwa shida kubwa kwa Benki ya Uingereza na kwa serikali ya Liz Truss.
Mfumuko wa bei umeongezeka hadi asilimia 10.1 kwa mwaka nchini Uingereza, kiwango cha juu zaidi katika miaka 40 na cha juu zaidi kati ya nchi za G7, na kuifanya kuwa shida kubwa kwa Benki ya Uingereza na kwa serikali ya Liz Truss. REUTERS - PAUL CHILDS
Matangazo ya kibiashara

Nepi, maziwa, mboga... Dora amejiwekea akiba ya mboga kwa ajili ya familia yake kubwa. "Sijui ilikuwa kiasi gani hapo awali, lakini huwa nanunua kitu kimoja na kujiuliza kwa nini ni ghali sana? Bei za bidhaa za maziwa, mchele zimepanda sana. Ningesema ninatumia angalau 20% zaidi, "amebaini mama huyo.

Kwa wastani, bei ya chakula imeongezeka kwa 15% katika mwaka mmoja. Miongoni mwa bidha zilizojikuta zikikabiliwa na ongezeko kubwa zaidi ni pamoja na maziwa, pasta na supu za makopo. Edward, anayefanya kazi katika duka la kompyuta, tayari amelazimika kubadili mazoea ya familia: “Katika chakula, tumelazimika kupunguza kiasi na ubora. Hapo awali, tulikuwa na milo mitatu au minne, sasa ni miwili.

"Benki ya chakula inatusaidia, sioni aibu"

Mzee wa miaka 50 bado anaweza kutumia benki za chakula, ambazo hazijawahi kuwa na mahitaji mengi. Sivyo ilivyo kwa Ruth, mama ya tineja, ambaye ana wasiwasi kuhusu majira ya baridi kali yanayokaribia: “Mwanangu hula sana. Benki ya chakula inatusaidia, sioni aibu. Wanatusaidia kwa mahitaji ya kimsingi: mkate, siagi, wakati mwingine maziwa kidogo na mayai”.

Mishahara imeongezeka kwa 5% tu kwa wastani. Hii ni nusu ya kiwango cha mfumuko wa bei. Kiwango cha kupanda kwa bei, ambacho kinasababisha chaguzi ngumu kuhusu uainishaji wa faida za kijamii na mishahara ya wafanyakazi wa umma au pensheni, inasumbua kazi ya Waziri Mkuu Liz Truss, ambaye sasa amebanwa vikali na ambaye lazima akabiliane na maandamano ya mara kwa mara ya Waingereza kwa ongezeko la mishahara. Kiongozi huyo wa Uingereza anapigania uhai wake wa kisiasa baada ya mpango wa bajeti uliowasilishwa Septemba 23 ambao ulichoma soko la fedha na kumlazimu kukabiliwa na hali ngumu kisiasa na fedheha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.