Pata taarifa kuu

Rais Macron akutana na mabalozi wa Ufaransa, awasihi kuhusu diplomasia ya Ufaransa

Takriban saa mbili za hotuba rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa minajili ya kufufua tena zoezi la kila mwaka la rais kukutana na mabalozi wa Ufaransa ambalo janga la UVIKO lilikuwa limezuia katika miaka ya hivi majuzi. Emmanuel Macron alizungumza Alhamisi hii asubuhi na mabalozi wanaowakilisha Ufaransa duniani. Fursa kwa rais malengo ya diplomasia ya Ufaransa.

Emmanuel Macron akiwahutubia mabalozi wa Ufaransa wanaowakilishi nchi hii katika nchi za kigeni, Alhamisi hii, Septemba 1, 2022.
Emmanuel Macron akiwahutubia mabalozi wa Ufaransa wanaowakilishi nchi hii katika nchi za kigeni, Alhamisi hii, Septemba 1, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya Emmanuel Macron ambayo imefungua siku mbili za semina, hotuba ambayo ilitawaliwa zaidi na vita vya Ukraine na matokeo yake. 'Sintofahamu', 'mpasuko', ni kwa maneno haya makali ambayo rais wa Ufaransa ameelezea hali ya ulimwengu. Ulimwengu wa migogoro: UVIKO, Tabia nchi na bila shaka uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. "Vita vya unyakuzi kwenye milango yetu, vikiongozwa na nchi yenye nguvu [yenye silaha za nyuklia] na mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa", kulingana na Emmanuel Macron.

... Vita vya unyakuzi kwenye milango yetu, vikiongozwa na nchi yenye nguvu, mjumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama, ikiungwa mkono na vita vya mseto vilivyowekwa katika kiwango cha kimataifa, na muundo wa kihistoria wa mifumo iliyowezesha kudhibiti utandawazi na uhusiano kati ya mataifa, hiyo ni vita inayoendelea nchini Ukraine. Na kwa hivyo, nasema hapa kwa nguvu kubwa kwa sababu ni mabadiliko makubwa kwa nchi yetu na diplomasia yetu. Wakati ambao tungeweza kutumaini kuvuna faida za amani umekwisha, na nadhani kwa muda mrefu, tutalazimika kuilinda na kuijenga upya. Wakati ambao tulifikiri tunaweza kufurahia uhuru wetu bila kulipa gharama umekwisha, ni lazima tuthamini uhuru wetu na maadili yetu, lakini tutalazimika kuvitetea, kuvipigania, na kukubali matokeo yote ambayo hii ina maana wakati wengine wanapigana kwa niaba yetu kwa ajili yao, hali ambayo inatokea leo nchini Ukraine. Na wakati ambapo utaratibu wa kimataifa, uliofafanuliwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, ulioimarishwa mwishoni mwa Vita Baridi, ulikuwa kiini cha uhusiano kati ya mataifa umeharibiwa, lazima tuujenge upya ...

Emmanuel Macron: vita vya Ukraine ni 'mpasuko'

Rais wa Ufaransa anasema mpasuko huu unahusisha mabadiliko makubwa kwa diplomasia ya Ufaransa. Anatoa wito kwa diplomasia  "kupambana". Kwa mujibu wa Emmanuel Macron, Ufaransa lazima itetee uhuru wake na ushawishi wake duniani. Ni lazima ifanyie kazi ubia na lazima ifanyie kazi umoja wa pande nyingi. Na lazima ichukue hatua kwa misingi mipya kama vile "mapambano ymbalimbali": propaganda, ushawishi na dhidi ya ushawishi kwenye mitandao ya kijamii ...

Wanadiplomasia wanaotumia mitandao ya kijamii

Rais wa Ufaransa ametoa wito wa "kuchukua mkakati wa ushawishi na kwa minajili ya Ufaransa", amehimiza "matumizi bora ya mtandao wa France Médias Monde, ambao ni muhimu kabisa, ambao ni lazima uwe nguvu kwetu". France Médias Monde inaleta pamoja kituo cha habari cha France 24 na redio RFI.

Nchi yetu mara nyingi hushambuliwa. Na inashambuliwa kwa maoni ya umma, na mitandao ya kijamii na kwa ghiliba. Na Afrika ni bara bora kwa hili. Kwa yote niliyosema hivi punde, nataka njia za chini zisitishwe. Ni kwa sababu tutakuwa na sera ya kweli ya ushirikiano ambayo inapitia utamaduni, michezo ambayo inakuza diaspora zetu. Tutaondoa masimulizi ya msingi ya Kirusi, Kichina au Kituruki ambayo yanawafafanulia kwamba Ufaransa ni nchi inayofanya ukoloni mamboleo na ambayo inaanzisha jeshi lake kwenye ardhi zao. Wakati fulani inatubidi tuvunje vipengele ambavyo tungeviacha wavitumie.

Emmanuel Macron: "Lazima tuwe wakali zaidi na tuhamasishwe" kuhusu vita vya habari

Emmanuel Macron amewasihi wanadiplomasia wa Ufaransa kuwa "watendaji zaidi" kwenye mitandao ya kijamii ili kujibu vyema mashambulizi ambayo Ufaransa inapitia kwa maoni ya umma, hasa barani Afrika: Ufaransa imekuwa ikilengwa na kampeni za upotoshaji nchini Mali, dhidi ya hali ya mvutano wa kidiplomasia kati ya Paris na Bamako. Habari nyingi za uwongo zilienea huko kama sumu mnamo 2021, zinazohusiana na vitendo vinavyodhaniwa vya wanajeshi wa Ufaransa nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.