Pata taarifa kuu

Ujerumani yapanga kutuma silaha mpya nchini Ukraine

Kansela Olaf Scholz ametangaza Jumanne kwamba Ujerumani inapanga kuwasilisha silaha mpya kwa Ukraine, zenye thamani ya zaidi ya euro milioni 500, chanzo kimeliambia shirka la habari la Reuters.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz. AP - Christian Charisius
Matangazo ya kibiashara

Mshiriki wa mkutano wa video kuhusu Ukraine uliofanyika Toronto, Canada, ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba Ujerumani inapanga kutoa mifumo mingine mitatu ya kupambana na ndege aina ya Iris-T, dazeni ya magari ya uokoaji yenye silaha, mifumo 20 ya kurusha roketi, zana za usahihi na mifumo ya kuzuia ndege zisizo na rubani.

Silaha hizo zitawasilishwa mnamo 2023, labda mapema, kimeongeza chanzo hiki, na kubaini kuwa wabunge wa Ujerumani bado walipaswa kuidhinisha mradi huu ambao Olaf Scholz alielezea kama mchango katika uboreshaji wa kisasa wa jeshi la Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.