Pata taarifa kuu
UFRANSA-AFYA

Ufaransa kuimarisha vita dhidi ya maambukizi ya monkeypox

Waziri wa afya nchini Ufaransa François Braun, amedhibitisha kuwa watu karibia 1,700 tayari wameambukizwa virusi vya monkeypox kwenye taifa hilo la bara ulaya.

Waziri wa afya wa Ufaransa -François Braun
Waziri wa afya wa Ufaransa -François Braun AFP - ALAIN JOCARD
Matangazo ya kibiashara

Waziri Braun aidha ameeleza kuwa serikali hadi kufikia sasa imefungua vituo 100 vya kutoa chanjo dhidi ya maambukizi ya monkeypox ambapo watu zaidi ya 6,000 wamechoma chanjo hiyo.

Wizara ya afya imetangaza kuwa itafanya uhamasishaji zaidi ilikuhakikisha kila raia anafikiwa na chanjo ikiwemo kuwapa mafunzo ya kuchoma chanjo hiyo wanafunzi wa udaktari.

Raia walio na dalili za ugonjwa huo nchini humo nayo wametakiwa kujitenga haraka iwezekanavyo ilikudhibiti msambao wa maambukizi hayo.

Aidha serikali ya ufaransa imetangaza kuwa itatoa nafasi kubwa kwa raia wake waliomo katika hatari kubwa ya kuambukizwa monkeypox wakati wa uchomaji chanjo.

Kwa mujibu wa waziri Braun, idadi kubwa ya maambukizi hayo imeripotiwa katika eneo la Paris ambapo amesema kuwa kituo cha kutoa chanjo kitaekwa wiki hii kuwasiadia wakaazi kupata huduma za kiafya.

Siku ya Jumamosi ya wiki iliyopita shirika la afya duniani WHO liltangaza maambukizi ya monkeypox kuwa janaga na la kiafya duniani.

Mwaka huu peke, watu zaidi ya 16,000 wamedhibitishwa kuaambukizwa katika mataifa 17 ya dunia, Bara Afrika likiwa limesajili vifo vya watu wa tano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.