Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE MAPIGANO

Mwanahabari wa Urusi Marina Ovsyannikova ameachiwa huru baada ya kuzuiwa

Mwanahabari wa Urusi Marina Ovsyannikova, ambaye alijipatia umarufu baada ya kulaani hatua ya Urusi kuivamia Ukraine, ametanagaza kuwa amechiwa baada ya kuzuiwa kwa saa kadhaa.

Marina Ovsyannikova, Mwanahabari wa Urusi.
Marina Ovsyannikova, Mwanahabari wa Urusi. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Wakili wake wanahabari huyo, Dmitri Zakhvatov, amesema kuwa alikuwa anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa madai ya kukosea jeshi heshima hatua ilionekana kama njia moja ya kumuunga mkono mwanaharakati wa upinzani Ilya Yashin, anayetuhumiwa kusambaza taarifa za uwongo kuhusu jeshi.

Baada ya kuwatuma wanaajeshi wake nchini Ukraine, Moscow ilibuni sheria inayoruhusu kuwafunga gerezani miaka 15 watu wanohusishwa na kusambaza taarifa kuhusu jeshi iwapo mamlaka zitabaini kuwa ni za uwongo.

Hadi sasa, Mamlaka nchini Urusi haijatangaza kuanzisha uchunguzi dhidi ya Ovsyannikova kwa kuhusishwa na uhalifu.

Hatua ya kuzuiwa kwa muda kwa mwanahabari huyo kumekuja baada yake kuandamana peke yake karibu na Kremlin, akiwa na mabango yaliokuwa yanaikashifu hatua ya jeshi la Urusi kuivamia Ukraine na rais Vladimir Putin.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.