Pata taarifa kuu
UFRANSA-SIASA

Ufaransa: Serikali ya rais Macron imepata pigo la kwanza bungeni.

Serikali ya Ufaransa imepata pigo la kwanza bungeni hatua inayokuja baada ya chama tawala chake rais Macron kupoteza idadi kubwa ya uungwaji mkono katika uchaguzi mwa mwezi uliopita.

Rais wa Ufaransa Emmanuel  Macron na waziri mkuu  Élisabeth Borne
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na waziri mkuu Élisabeth Borne © AP/Christophe Petit Tesson
Matangazo ya kibiashara

Bunge la kitaifa usiku wa kuamkia jumanne lilikataa kuidhinisha muswada unaotaka kuipa serikali mamlaka ya kuwataka wasafiri kuwasilisha vyeti vya kudhibitisha iwapo hawana maambukizi ya uviko 19 au wamechanjwa kabala ya kuingia nchini Ufaransa.

Wabunge 219 kutoka vyama vya upinzani walipiga kura kupinga muswada huo dhidi ya wabunge 195 wa chama tawala. Vyama vya upinzani hapa vikiungana kuangusha muswada huo.

Waziri mkuu Elisabeth Borne, amepinga hatua hiyo ya wapinzani kuweka nguvu pamoja kuangusha mapendekezo ya serikali. Baadhi ya wabunge wanaomunga mkono rais Macron nayo pia wakieleza kusikitishwa na swala hilo.

Licha ya muswada huo kupingwa bungeni baadhi ya mambo muhimu ya kabiliana na wimbi la saba la maambukizi ya uviko 19 yalipitishwa na wabunge baada ya kupata kura 221 dhidi ya 187.

Wachambuzi wa siasa za Ufaransa wanahoji kuwa Macron atahitajika kuwashawishi wabunge 62 wa Republicans kutoka katika mrengo wa kulia kwa minajili ya kupitisha misuada muhimu ya serikali bungeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.