Pata taarifa kuu
MAREKANI- SIASA

Marekani: Joe Biden kufanya ziara mashariki ya kati wiki hii.

Rais wa Marekani, Joe Biden, juma hili anaanza ziara ya kutembelea nchi za mashariki ya Kati, ikiwemo nchi za Israel na Saudi Arabia ambako amekosolewa kwa kupuuza rekodi mbaya ya haki za binadamu kwenye taifa hilo.

Rais wa Marekani- Joe Biden.
Rais wa Marekani- Joe Biden. © 路透社图片
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya rais Biden Mashariki ya kati, imeonekana kisiasa kufungua ukurasa mwingine wa kupungua kwa ushawishi wa Marekani katika mataifa ya eneo hilo.

Hivi leo Biden atazuru Israel ambapo atatumia muda mchache katika maeneo yanayokaliwa na wapalestina, kabla ya kuelekea Saudi Arabia ambako atahudhuria kilele cha mkutano wa viongozi wa falme za kiarabu, pamoja na viongozi kutoka Jordan, Misri na Iraq.

Tofauti kati ya Saudi na Marekani ziliongezeka, wakati Rais Biden katika hatua zake za kwanza kuchukua madaraka, alichapisha ripoti ya kijasusi ambayo ilisema kwamba Mrithi wa ufalme wa Saudi, Mohammed bin Salman, alihusika na mauaji ya mwandishi wa habari wa Saudi Jamal Khashoggi, mjini Instabul mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.