Pata taarifa kuu
UKRAINE- URUSI

Marekani: Iran inapanga kuihami Urusi na ndege zisizo na rubani.

Nchi ya Iran inapanga kuisambazia Urusi mamia ya ndege zisizo na rubani kwa ajili ya matumizi katika mapambano yake dhidi ya Ukraine, baadhi yake zikiwa na uwezo wa kushambulia, Marekani ikionya kuhusu hatua hii ya Iran.

Ndege zisizo na rubani zinazomilikiwa na Iran.
Ndege zisizo na rubani zinazomilikiwa na Iran. VIA REUTERS - WANA NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa White House kuhusu masuala ya kiusalama Jake Sullivan katika taarifa yake anasema marekani imepokea ripoti za kiitelenjisia kuwa Iran inapanga kutoa mafunzo ya kutumia ndege hizo kwa wanajeshi wa Urusi.

Aidha Washington, haijabainisha iwapo tayari Iran imewasilisha ndege hizo nchini Urusi.

Mataifa ya Urusi na Ukraine yamekuwa yakitegemea pakubwa ndege zisizo na rubani katika vita dhidi ya pande hizo mbili katika mzozo unaoendelea.

Hatua ya Iran inatajwa kuja ikiwa imepita wiki moja tu tangu Ukraine nayo itoe ombi la kutaka kusaidiwa na ndege hizo kama njia moja na kupiga jeki vita dhidi ya Urusi.

Vile vile ripoti ya Marekani inaeleza kuwa ndege zisizo na rubani zinazomlikiwa na Iran, awali zimetumiwa na waasi wa Houthi nchini Yemen kuishambulia Saudi Arabia.

Matamshi ya Washington yanakuja wakati huu ambapo rais Joe Biden anatarajiwa kufanya ziara katika mataifa ya Israeli na Saudi Arabia wiki hii. Iran ni baadhi ya nchi ambazo hazijajitokeza kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Marekani na washirika wake wametoa mchango wa silaha zenye mabilioni ya dolla za nchi hiyo kiuhami Ukraine tangu kuvamiwa na Urusi mwezi Feburuari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.