Pata taarifa kuu
UFRANSA-SIASA

Rais Macron yuko chini ya shiniko kueleza uhusiano wake na texi za Uber.

Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron anapata shinikizo kufafanua ni kwa nini aliamua kuunga mkono application ya usafiri ya Uber, wakati alipokuwa Waziri wa uchumi.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Uchunguzi uliofanywa na Gazeti la  Le Monde la Ufaransa na The Guardian la Uingereza, umeonesha kuwa  Macron alipokuwa Waiziri alikuwa na mikutano ambayo haikuwa rasmi na viongozi wa Uber kati ya mwaka 2014 hadi 2016 na kuwaahidi kuwaisaidia ili kuingia kwenye soka la Ufaransa.

Nyaraka zilizofuja kama ujumbe mfupi kati ya Macron na Wakurengzi wa kampuni hiy oya usafirishaji zinaonesha kuwa, aliingia katika mkataba wa siri katika kipindi ambacho kuwa na pingamizi kubwa ya kuanzisha usafiri wa uber ambao ungeua teksi za kawaida.

Katika mkataba huo wa siri, Macron aliahidi kuisaidia Uber kuingiliana na sheria iliyoazishwa mwaka 2014, iliyolenga kudhubiti application za texi nchini Ufaransa.

Wabunge wa upinzani wamemshtumu rais Macron kuhusu hatua hiyo wakisema aliunga mkono uwekeaji wa sekta binafsi ya kigeni bila ya kuwashirikisha mawaziri wengine.

Bungeni, serikali ya Macron chini ya Waziri Mkuu Elisabeth Borne inatarajiwa kukabiliwa na kura ya kuikosa imani naye, lakini inatarajiwa kutiopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.