Pata taarifa kuu
URUSI-UKRAINE

Mji wa Mykolaiv nchini Ukraine washambuliwa na wanajeshi wa Urusi

Mji wa Mykolaiv nchini Ukraine, umeshuhudia mashambulio ya bomu yenye nguvu mapema leo, baada ya watu 21 kuuawa kufuatia shambulio lililolenga jimbo la Odeda.

Shambulizi katika  Mykolaiv
Shambulizi katika Mykolaiv REUTERS - EDGAR SU
Matangazo ya kibiashara

Mashambulio hayo yamesababisha kuharibiwa kwa kambi tano za jeshi la Ukraine katika mji huo, huku yakilenga pia maeneo matatu ya kuhifadhi silaha za kijeshi.

Meya ya mji wa Mykolaiv amewaambia wakaazi kusalia majumbani mwao, kufuatia mashambulio hayo yaliyosikika kuanzia Jumamosi asubuhi.

Urusi inakanusha madai ya kulenga makaazi ya raia na badala yake inalenga vituo vya kijeshi wa Ukraine.

Wakati uo huo, wapiganaji wanaounga mkono wanajeshu wa Urusi katika jimbi la Luhansk, wanadai kuuzunguka mji wa Lysychansk, Mashariki mwa Ukraine.

Marekani nayo inasema inatuma mtambo maalum wa kuzuia makombora, miongoni mwa silaha nyigine, kuisaidia Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.