Watu zaidi ya 20 wauawa nchini Ukraine baada ya kushambuliwa na jeshi la Urusi
Watu zaidi ya 20 wameuawa wakiwemo watoto wawili baada ya jeshi la Urusi kurusha kombora katika makaazi ya watu Kusini Magharibi mwa jimbo la Odesa nchini Ukraine.
Imechapishwa:
Maafisa wa serikali nchini Ukraine wamesema kombora la Urusi lililenga jumba moja lenya maakazi la orofa 9 na mkahawa na na kuwaua 19 hao mbali na kusabisha moto mkubwa, ambpo shughuli za kuwaoakoa waliokwama kwenye vifusi zilianza amara moja.
Jeshi la Ukraine limetuhumu Urusi kwa kutumia makombora kushambulia miji yake katika mashambulizi yake ya hivi karibuni, likiwemo shambulizi la Kremenchuk ambapo watu 18 walifariki na lile la jiji la Kyiv jumapili iliopita.
Andriy Yermak mkuu wa wafanyakazi katika afisi ya rais wa Ukraine, amefaninisha tukio la Ijumaa na magaidi amabao wameshindwa katika uwanja wa mapambano na sasa wanawashambulia raia ambao hawana hatia.
Hata hivyo msemaji wa Krimlin, Dmitry Peskov, amekanusha taarifa za jeshi la Urusi kushambulia raia akisema wanajeshi wa Urusi siku zote hawafanyi kazi na raia.