Pata taarifa kuu

Nchi za NATO kuongeza vikosi vyake hadi zaidi ya wanajeshi 300,000

Viongozi wa NATO wataamua katika mkutano wa kilele wa Madrid, Jumatano Juni 29, kuongezq nguvu zao za kujihami na kuongeza wanajeshi wake hadi zaidi ya 300,000 katika kiwango cha juu cha maandalizi ili kukabiliana na tishio hilo kutoka Urusi. amesema Katibu Mkuu wa Muungano huo.

Kutoka kushoto, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel mbele ya meza ya pande zote huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akionekana kwenye televisheni kuwahutubia viongozi wa G7.
Kutoka kushoto, Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, Rais wa Marekani Joe Biden, Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel mbele ya meza ya pande zote huku Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy akionekana kwenye televisheni kuwahutubia viongozi wa G7. AP - Kenny Holston
Matangazo ya kibiashara

"Pia tutajenga uwezo wetu wa kuwa na nguvu zaidi katika tukio la migogoro, tukiwa na vifaa vilivyowekwa tayari, uwezo ambao utakuwa umetumwa mbele, kama vile ulinzi wa anga, na vikosi vilivyopewa jukumu la kutetea baadhi ya washirika," ameongeza Mnorwe Jens Stoltenberg, akinukuliwa. na shirika la habario la AFP.

Wakati huo huo Viongozi wa nchi 7 tajiri duniani wameahidi kutenga kiasi cha dola bilioni 600 kwa ajili ya kujenga miundo mbinu ya kupamabana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Mradi huo unazingatiwa kuwa jibu la nchi za magharibi kwa uwepo wa China katika nchi zinazoendelea.

Mwenyeji wa mkutano wa nchi hizo tajiri kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema nchi za G7 zitafanya juhudi za kujenga ushirikiano wa karibu na nchi zinazoendelea ikiwa ikiwa pamoja na bara la Afrika. Kansela wa Ujerumani ameeleza kuwa nchi saba tajiri zinakusudia kujenga ushirikiano na nchi zinazoendelea siyo kwa ajili ya hisani tu bali kwa ajili ya manufaa ya pande zote.

Kwa upande wake rais wa Marekani Joe Biden  amesema vitega uchumi vitakavyowekwa vitaelekezwa katika kuimarisha uchumi wa nchi zote na kwa ajili hiyo Marekani imeahidi kutenga dola bilioni 200 katika kipindi cha miaka mitano ijayo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.