Pata taarifa kuu

Waziri wa Uchumi wa Ujerumani aonya juu ya kufungwa kwa viwanda kwa ukosefu wa gesi

Ujerumani inaelekea katika uhaba wa gesi ikiwa usambazaji wa gesi ya Urusi utaendelea kuwa katika kiwango cha chini cha sasa. Baadhi ya viwanda vinaweza kulazimika kufunga ikiwa bidhaa hii itakuwa haitoshi msimu ujao wa baridi, Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Robert Habeck amesema katika mahojiano na makala ya Gazeti la Spiegel yaliyochapishwa leo Ijumaa.

"Kuanzia sasa, kila mtumiaji wa gesi - kutoka kwa makampuni hadi kaya binafsi - watalazimika kupunguza matumizi yao iwezekanavyo ", Waziri wa Uchumi Robert Habeck alisema Machi 30.
"Kuanzia sasa, kila mtumiaji wa gesi - kutoka kwa makampuni hadi kaya binafsi - watalazimika kupunguza matumizi yao iwezekanavyo ", Waziri wa Uchumi Robert Habeck alisema Machi 30. © REUTERS/Michele Tantussi
Matangazo ya kibiashara

"Kampuni zinaweza kulazimika kusitisha uzalishaji, kuachisha kazi wafanyakazi,  usambazaji unaweza kusitishawa, familia nyingi zinaweza kuingia kwenye deni kwa kutolipia bili za gesi na kuwa masikini," Robert Habeck ameliambia gazeti hilo, akibaini kwamba hali hii ni sehemu ya mkakati wa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kuigawanya nchi.

Hili linachochea "hali mbaya kwa watu anaoshawishika haraka kwa lengo la kuhatarisha demokrasia", amesisitiza, akiongeza kuwa ni muhimu kukwamisha mipango ya Vladimir Putin.

Katika muktadha huu, Robert Habeck amebaini kuwa na matarajio ya hatua mpya za usaidizi zilizokusudiwa kwa biashara na familia, huku akionya kwamba msaada huu hautafanya uwezekano wa w akukabilianan na hali hii, limeripoti Gazeti la Spiegel.

Kwa upande wake, mkuu wa Bundesnetzagentur, mdhibiti wa masoko ya gesi nchini Ujerumani, Klaus Müller, ametangaza leo Ijumaa kwenye televisheni ya ARD kwamba watumiaji wanaweza kukabiliwa na mara mbili au hata mara tatu ya bili zao za nishati. Baadhi tayari wameona ongezeko la kati ya 30% na 80% ikilinganishwa na mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.