Pata taarifa kuu

Ufaransa: Waziri Mkuu ajiuzulu, Macron akataa

Waziri Mkuu wa Ufaransa Elisabeth Borne amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Emmanuel Macron, ambaye amepinga kujiuzule kwake "ili serikali iweze kuendelea na majukumu yake na kuchukua hatua katika siku sijazo", ikulu ya Elysée imetangaza leo Jumanne asubuhi.

Waziri Mkuu Élisabeth Borne amewasilisha barua yake ya kujiuzulu mnamo Juni 21, 2022 kwa Emmanuel Macron, ambaye amepinga kujiuzulu kwake.
Waziri Mkuu Élisabeth Borne amewasilisha barua yake ya kujiuzulu mnamo Juni 21, 2022 kwa Emmanuel Macron, ambaye amepinga kujiuzulu kwake. AFP - GONZALO FUENTES
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Jamhuri atafanya "mashauriano muhimu ya kisiasa (...) ili kubaini suluhisho zinazowezekana katika kuwahudumia  Wafaransa", Ikulu ya Elysée imebainisha, kabla ya mfululizo wa mikutano na viongozi wa vyama vya siasa siku ya Jumanne na Jumatano katika ikulu ya Elysée.

Kiongozi wa serikali, Élisabeth Borne atakutana kwa mazungumzo na serikali nzima mapema alasiri katika ofisi yake Matignon.

Viongozi sita wa kisiasa watapokelewa mtawalia leo na rais Emmanuel Macron kutafuta "suluhu zinazoweza kujenga", kulingana na taarifa ya Élysée: Christian Jacob kutoka chama cha Les Républicains) atafungua mashauriano hayo saa nne asubuhi., kabla ya Olivier Faure (Chama cha Kisoshalisti) saa tano mchana, François Bayrou (chama cha Kidemokrasia) saa nane mchana, Stanislas Guerini (chama cha Renaissance) saa tisa alaasiri, Marine Le Pen (chama cha RN) saa kumi na moja na nusu na Fabien Roussel (Chama cha Kikomunisti) saa kumi na mbili jioni.

Mashauriano hayo yataendelea siku ya Jumatano ambapo rais a Ufaransa atawapokea kiongozi wa chama cha kijani (Les Verts), Julien Bayou, kiongozi nambari mbili wa chama cha La France insoumise (LFI), Adrien Quatennens, na kiongozi  wa kundi la LFI katika Bunge la Kitaifa, Mathilde Panot.

Adrien Quatennens na maafisa wengine kadhaa wa LFI wametaka kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Élisabeth Borne, ambaye hatakuwepo kwenye mikutano na vyama vya kisiasa. Kaimu kiongozi wa chama cha RN Jordan Bardella amebaini kwamba Waziri Mkuu Élisabeth Born atalazimika "kuachia ngazi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.