Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Kyiv yatarajia Urusi 'kuongeza mashambulizi'

Siku ya 117 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumatatu Juni 20, ni wiki ya "kihistoria" inayoanza, kulingana na maneno ya rais wa nchi hiyo Volodymyr Zelensky.

Moshi ukifuka kutoka jiji la Sievierodonetsk katika eneo la Donbass mashariki mwa Ukraine mnamo Juni 13, 2022.
Moshi ukifuka kutoka jiji la Sievierodonetsk katika eneo la Donbass mashariki mwa Ukraine mnamo Juni 13, 2022. AFP - ARIS MESSINIS
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi na Ijumaa, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zitaamua juu ya hali ya Ukraine kuwania kuwa mwanachama wa Umoja huo. Kwa hivyo, kwa kutarajia tarehe hii ya mwisho, rais wa Ukraine anatarajia Moscow "kuongeza mashambulizi yake wiki hii".

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya nchi za Magharibi, NATO, anahofia kuwa vita vya Ukraine vitadumu kwa muda mrefu. "Tunapaswa kuwa tayari kwa vita hivi kudumu kwa miaka kadhaa," Jens Stoltenberg ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild.

Akirejea kutoka katika ziara ya eneo la kusini, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesisitiza kwamba nchi yake "itarejesha kila kitu" katika maeneo ambayo jeshi la Urusi linashikilia.

Kufuatia uwezekano wa Ukraine kujiunga na Umoja wa Ulaya, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametaja maoni mazuri ya Tume ya Ulaya kama "mafanikio ya kihistoria", akisubiri uamuzi wa Baraza la Ulaya wiki ijayo. "Tutafanya kila kitu ili kufanya uhusiano wetu na Ulaya kuwa thabiti iwezekanavyo," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.