Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa wabunge Ufaransa: Baadhi ya vyama vyapoteza na vingine vyafaulu

Vyama vikuu vya kisiasa nchini Ufaransa vilikuwa vikicheza dau kubwa kwa uchaguzi huu wa wabunge mwaka wa 2022, lakini matokeo ya hayakukidhi matarajio yote, baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa wabun Jumapili Juni 19, 2022.

Taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wabunge iliyochapishwa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa.
Taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wabunge iliyochapishwa na wizara ya mambo ya ndani ya Ufaransa. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Bunge la kitaifa limepata wajumbe wapya na baadahi ya vyama vya siasa vimepoteza viti na vingine vimefaulu zaidi kuliko hapo awali. Haya ndiyo yale ambayo makadirio ya matokeo ya duru ya pili ya uchaguzi wa wabunge wa mwaka 2022 yanapendekeza: muungano wa rais haujafanya vizuri katika uchaguzi huo, mrengo wa kushoto umepoteza mara mbili ikilinganishwa na miaka mitano iliyopita, mrengo wa kulia umepoteza vit vingi, na chama cha Les Républicains kimefanya vizuri. Hakuna chama au muungano uliyopata idadi ya kutosha ya viti vinavyohitajika ili kuwa na wingi wa viti katika bunge hilo. Kwa sasa vyama vyote bungeni vitalazimika kushirikiana kwa pamoja, vikitia mbele idadi ya viti vilivyopata.

Muungano wa Ensembe, wapoteza

Chama cha rais (ex-LaREM), kilichokuwa na idadi kubwa ya viti katika bunge lililomaliza muda wake, kiliunda muungano uuitwao Ensemble!, kwa ushirikiano na vyama vya MoDem na Horizon kwa matumaini ya kupata ushindi mkubwa katka uchaguzi huo. Rais Emmanuel Macron alipoona hali imebadilika baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi, siku ya Jumanne Juni 14 alionya kwenye uwanja wa ndege wa Orly, kwamba "Jumapili, hakuna sauti itapotezwa kwa chama cha Rebublique". Akimaanisha muungano wake. Kwa makadirio ya Jumapili hii jioni, muhula wa pili wa miaka mitano wa Rais wa Jamhuri unaanza na mzozo wa kisiasa, baada ya miaka mitano iliyoangaziwa na mizozo ya kijamii na kiafya.

Mabadiliko yanapaswa kufanyika katika siku zijazo: mawaziri walioshindwa, kama vile Brigitte Bourguignon (Waziri wa Afya) au Amélie de Montchalin (Waziri wa Ikolojia), watalazimika, kulingana na sheria ambayo haijatamkwa, kujiuzulu serikalini. Waziri Mkuu Elisabeth Borne anatarajia kutangaza baraza jipya la mawaziri. Badala ya muungano wa Nupes au chama cha RN, kuna nafasi nzuri kwambavitajiunga na Les Republicains kuwa na wabunge zaidi ya 289 na kupata kura ya imani ya Bunge.

Changamoto nyingine: kudumisha muungano wa rais kwa miaka mitano. Kama tulivyotaja katika makala iliyotangulia, kuna uwezekano wa kuwepo na hatari ya kutengana mwaka mmoja au miwili kabla ya mwisho wa muhula wa miaka mitano. Chama cha Horizon,  cha Édouard Philippe, kinaweza kujaribu kujitofautisha na chama cha rais ili kujiandaa kwa uchaguzi wa urais wa mwaka 2027.

Muungano wa  Nupes, wapoteza baadhi ya viti

Muungano wa mrengo wa kushoto hautakuwa na idadi kubwa ya wabunge 289, ambayo ingewezesha Jean-Luc Mélenchon kuchukuwa nafasi ya waziri mkuu. Sura ya mwanasiasa huyo, ambaye wakati mwingine huwagawanya hata miongoni mwa wafuasi wa mrengo wa kushoto, ilikuwepo kila mahali kwenye mabango ya kampeni ya wagombea wa muungano wa Nupes. Duru ya kwanza ilishuhudia muungano huo ukivuka wingi wa kura za urais kwa makumi ya maelfu ya kura, lakini idadi ya kufikia nafasi ya waziri mkuu huko Matignon, iliyotangazwa haikutosha.

Hata hivyo, Jean-Luc Mélenchon amefaulu katika duru ya pili ambapo hakuna aliyeamini baada ya kuraruliwa kwa upande wa kushoto katika uchaguzi wa urais. Alileta pamoja vyama vikuu vya mwelekeo wake katika muungano, ambao haukufanyika kwa miaka 25. Wanachama wa kushoto (Nupes + wapinzani) zaidi ya mara mbili ya idadi ya wabunge wake ikilinganishwa na mwaka 2017.

Kwa jumla muungano wa Nupes umepata viti 131, chama cha DVG kimepata viti 22, muungano wa Ensemble wa rais Emmanuel Macron umepata viti 245, chama cha LR kimepata viti 61, chama cha DVD kimepata viti 10, chama cha RN kimepata viti 89 na vyama vingine vimepata viti 19; hayo ndio matokeo ya uchaguzi wa wabunge kulingana na tarifa ya wizara ya mambo ya ndani ya ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.