Pata taarifa kuu

Ukraine: Lysychansk yajiandaa kwa vita

Shambulio la kombora la Urusi mnamo Alhamisi liliua watu wanne waliokuwa wamekimbilia katika Nyumba ya Utamaduni huko Lyssytchansk, Donbass. Na sasa jiji hilo linajiandaa kwa mapigano yanayoweza kutokea mitaani, huku vikosi vya Urusi vikipambana na wanajeshi wa Ukraine katika mji wa Severodonetsk, ulioko ng'ambo ya Mto Donets.

Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katikati, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakitembea kwenye uwanja ambapo magari ya kijeshi ya Urusi yaliyoharibika yanaonyeshwa mjini Kyiv, Ukraine, Ijumaa, Juni 17, 2022.
Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Ukraine, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, katikati, na Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakitembea kwenye uwanja ambapo magari ya kijeshi ya Urusi yaliyoharibika yanaonyeshwa mjini Kyiv, Ukraine, Ijumaa, Juni 17, 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Facebook, Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov alisema alifurahishwa wakati wa mkutano wa kilele huko Brussels baada ya kuhakikishiwa na washirika wa Muungano wa Atlantic kwamba Ukraine tayari inafanya sehemu ya familia ya NATO.

Hata hivyo, maoni haya hayajathibitishwa na Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg. Je, Ukraine tayari inajiona kama mwanachama halisi wa NATO? Hapana, kulingana na Vincent Desportes, jenerali wa jeshi la Ufaransa na mshauri mtaalam wa kijeshi, alipohojiwa na Heike Schmidt.

Kujiunga na NATO, kuna mchakato mrefu wa uanachama. Kwa hiyo ni mapema sana leo kusema kama Ukraine ni mwanachama wa NATO. Tunajua vizuri kwamba hii labda ni moja ya vipengele vya mazungumzo ambayo tutalazimika kuwa nayo siku moja na Bw (Vladimir) Putin, na kwa hiyo hakuna mtu leo ​​anaweza kuendeleza uwezekano huu ambao, kwa maoni yangu, itachukuwa miaka kadhaa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.