Pata taarifa kuu

Viongozi wa EU waahidi kumuunga mkono Volodymyr Zelensky

Viongozi wa mataifa ya Umoja wa Ulaya wameunga mkono mchakato wa Ukraine kuwa mwanachama wa Umoja huo, baada ya kutembelea jijini Kiev na kufanya mazungumzo na rais Volodymyr Zelensky.

Kutoka kushoto, Rais wa Romania Klaus Iohannis, Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani wanahudhuria mkutano katika ikulu ya Mariyinsky mjini Kyiv, Ukraine, Alhamisi, Juni 16, 2022.
Kutoka kushoto, Rais wa Romania Klaus Iohannis, Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani wanahudhuria mkutano katika ikulu ya Mariyinsky mjini Kyiv, Ukraine, Alhamisi, Juni 16, 2022. AP - Natacha Pisarenko
Matangazo ya kibiashara

Jana Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi wote kwa pamoja walisema wanaunga mkono Ukraine kuingia kwenye Umoja wa Ulaya. 

Rais Macron amewasifu wanajeshi wa Ukraine kwa kuendeleza mapambano dhidi ya wanajeshi wa Urusi. 

Wakizungumza na waandishi habari rais Macron alisema mataifa hayo manne yanafanya kila linalowezekana kuhakikisha Ukraine haitosimama peke yake kwenye vita dhidi ya Urusi.

Mbali ya msaada ziada wa silaha uliotangazwa na rais Macron, viongozi wa mataifa hayo manne pia wametangaza kuiunga mkono azma ya Ukraine ya kuomba kuwa mwananchama wa Umoja wa Ulaya

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.